Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ndugu tegemezi

Mind your Ughaibuni business...

 Nakumbuka miaka michache nyuma nilipokuwa Twita alijitokeza Binti mmoja nakuanza kuwaambia watu wa Ughaibuni(Nchi za Ulaya na Marekani) kuachana na Siasa za Tanzania na kufurahia maisha yako "mazuri" popote walipo Ulaya(popote nje ya Afrika)....natabua kua sio kila mtu Ulaya ana maisha mazuri(inategemea sababu yako ya kuishi huko) lakini nakubaliana nae. Wabongo wengi walimkandya/ponda kwa kudai kuwa anataka attention ya Bongo Twita sababu hakuna mtu anamfahamu, binti alijitetea na kusimamia alichokisema ambacho hakika nakubaliana nae. Watu wa Ughaibuni ambao hawaishi Tanzania  wanaguswa na Mabadiliko ya kisisa yanayoendelea Tz, hawa ni wachache sana ambao wana Biashara na pengine kumiliki ardhi(nyumba, mshamba n,k,) na wachache ambao hurudi nyumbani mara kwa mara, wengine wapo wapo tu na ndio huwa na kelele zaidi kuhusu Tanzania na Siasa zake. Unadhi utabadilisha nini  Tz na Kodi hulipi? Mind your Ughaibuni business and enjoy your High tax, cost of living and free Heathcare

Kila Familia/Ukoo ina mtu huyu...

  ...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje... Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa. Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama  ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume(ina