...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje...
Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa.
Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume(inategemea na ujinsi awenu)...kila msichana/mvulana unaemtaka, anakupiku anamchukua yeye au anakukatisha tamaa so unaachana nae na hivyo kupoteza kipusa/mshikaji. Kama ni watu wazima na mpo ndoani haoni shida kulala na mkeo/mumeo.
Mtu huyu huchagua mtu mmoja kati yetu kuwa "kipenzi" chake kwenye familia ili aweze kumtumia kama mficha siri wake na vile vile kumuonea....sasa kama wewe ni mdogo unaweza kudhani kuwa ni upenzo wa Kaka/Dada kwasababu ni mkubwa, utagundua kuwa yeye hakutunzii siri zako. Mara zote wewe ndio uishia kupata adhabu badala yake. Hii sio katika utoto tu bali mpaka utu unzima(ni).
Mwanadamu huyu huwa mwepesi sana kusaidia na kubeba mizigo ya matatizo ya wanafamilia wengine ktk mgongo wa kuwasaidia(anachotaka ni sifa na kuwa saviour) . Ni bingwa wa kutoa ahadi ili kama "Ukoo" muendelee na kuishi maisha mazuri kama yeye, anawakusanya na kuwaambia mje na Wazo la biashara ambalo litafanyiwa kazi na kuwa Kampuni halafu yeye atali-fund, lakini hatimizi ahadi hiyo (akijua wazi sio rahisi kukubaliana kwasababu kila mmoja wenu na familia yake ana-idea zake zinazoendana na familia yake) kwasababu ninyi wote hamna ushirikiano...so hamfanikinwi na ni fault yenu.
Dada/Kaka huyu uhakikisha anasaidia kila mtu mwenye shida kwenye Ukoo/familia lakini kamwe hatokusaidia ili ujisaidia, atakusaida enough to sort your shida out kwa muda fulani then go back to ask for more help(atakupa vema tu ili uendelee kumtegemea)....kamwe hatokupa nyavu ukavue samaki wako mwenyewe bali atakupa Samaki(sounds kama EU/US na Nchi za Afrika eti?)
Husabaisha drama kwenye familia, lakini huwa hakuna wa kumuweka sawa...kila mtu ana "muheshimu", maana ukijitia unajua sana na kumkandamiza ujue hutopata msaada kutoka kwake. Ukifanikiwa kumpinga basi utapatiwa kikao chako peke yako usutwe....unaendaje kinyume na "Mungu" wa familia?
Yeye ni victim wa kudumu, kila mtu anamchukia, kila mtu hampendi yeye, kila mtu anataka kumuharibia, wote mnamuonea wivu. Na ikiwa wewe umeondoa mavumbi na umeamua kujitoa na kumchukulia kama mwanadamu tofauti na wengine ukooni/familiani basi atakuchafua kwa kila ndugu na rafiki zako, utabebeshwa mizigo ya lawama na ikiwa umeoa/olewa basi Mkeo/Mumeo ndio atakuwa sababu kuu kwanini "unamchukia" yeye, mkeo/mumeo kakubadilisha! Ukweli ni kuwa huna chuki ila wewe hupendi tu kubabaikia/shuku wanadamu wenzio.
Usipokuwa makini kwenye mahusiano yako ya kimapenzi na shughuli nyingine kwa maendeleo yako binafsi wakati bado unahusiano mzuri na nduguyo huyo ambae anajiona ni "Mungu" kwenye Ukoo/Familia yenu basi ujue hautofanikiwa, atatumia kila aina ya mbinu kuhakikisha humfikii na wala humpiti na huchukui nafasi yake aliojipa kwenye Ukoo/familia yenu.
Hyuu! nimechoka, maana yapo mengi. Nitakuona ukinona tena Wiki ijayo?
Bai.
Comments