Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kila kitu mie

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?  Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi". Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa

Tangu umefunga ndoa, ume-improve...

 ..Mchezo au upo vile vile? Kwamba ya nini ni-showcase  au ujiboreshe wakati  umeshampata, ni wako mpaka kifo? Sio sasa ni wangu wacha ni practise nae zaidi na time to time ni showcase niliyofuzu? nayo hapana? Ndoa ikibuma je utaanza kujifunza upya?  hehehehe hawa wa siku hizi hawajui kusubiri, yaani hata muda wa ku-show off maujuzi hupewi.....ukitoka na hujalipia  meal, umeachwa(wakati haukuwa na uhusiano nae)....hii kwa wote, wewe na mkeo/mmeo.  Natambua kuna kubadilika au tuseme kukua(inategemea na umri mliofunga ndoa)....uboreshaji  wa tabia au mtindo wa maisha ni jambo muhimu, maana huwezi kuishi kama kijana/binti wa miaka 32 wakati sasa una miaka 47...Wataalamu wanasema kuwa Uhusiano haubadiliki bali wenza ndio hubadilika, mimi nabisha kwasababu ninyi mkibadilika/kua ni wazi kuwa mahitaji yenu yanabadilika na hivyo uhusiano mzima kubadilika.  Mfano; Uhusiano wenu ulivyokuwa kabla ya kufunga ndoa ni tofauti na sasa mmefunga ndoa, na uhusiano huu baada ya ndoa hubadilika baada ya k

Kila Familia/Ukoo ina mtu huyu...

  ...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje... Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa. Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama  ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume(ina

Marehemu....

Mungu aendelee kuwapa Mwanga wa Milele, Amina......hebu ngoja kwanza!! Wameenda wakiwa "wamelala" sasa mwanga wanini wakati wamelala? Ile kasumba ambayo mimi naona ni ubinafsi au kutafuta/taka kuonewa "huruma".....yaani marehebu baba blablabla....Marehemu sijui nani blablabla. Marehemu Baba wa Taifa anatuangalia na kugalauka Kaburini......yaani aache kufanya yaliyomuhimu huko aliko abaki kutuangalia sisi huku na kugalauka kutokana na ujinga au makosa na shida zetu! Sidhani kama hao marehemu huwa hata wanatuombe tulio hai tuendelee kupata "kiza" cha milele ili tusiamke na kukabiliana na shida za Dunia. Mtu akienda, ameenda na huna budi kukubali kuwa kaenda na anaendelea na maisha mengine bila wewe....dizaini ukifa unasahau all bout Dunia na watu wake.....Mambo ya new start...new life. Si wanasema unakuwa "declared dead only" kama Ubonko (Ubongo) haufanyi kazi, sasa kama Ubonko haufanyi kazi kumbukumbu za ya Duniani watazitoa wapi? (In my