...Kikao cha familia, hakianzi mpaka Dada/Kaka aje... Kwenye kila familia (hasa kama mpo wengi) huwa kunakuwa na ndugu mmoja ambae anajipa cheo na anataka abaki pale kwa njia na namna yeyote ile. Achana na wale ndugu wakubwa ambao automatically wanapewa "uongozi" na Wazazi...kuna yule mmoja wenu huibuka tu na kuanza kujiona ndio mwenye akili, ndio fashionable, Mfuata maadi, anajua kila kitu maishani, anafahamiana na watu wenye Majina(maarufu/viongozi), Msomi n.k, mara nyingi huwa mtoto wa Tatu mpaka Tano hivi kuzaliwa. Huyu mtu huangalia mapungufu kwenye familia halafu ana pursue kitu ambacho kitamfanya awe tofauti na ninyi wote. Kama ni Elimu basi atasoma kwa bidii na juhudi zote ili awapite wote, kama ni mafanikio kiuchumi atakuwa juu zaidi ya wote humo familiani(hii itampa nguvu ki-social hasa kwenye mikutano ya familia), likija suala la marafiki, yeye atakuwa ni rafiki zaidi kwa marafiki zenu wote ila rafiki zake ni wake peke yake...kwenye suala la wanawake/wanaume(ina