Skip to main content

Posts

Showing posts with the label rohombaya

Adui mpende.....mpende adui yako.

Hivi wewe una adui? Kusema ukweli kabisa mie sina adui which means mie sio adui wa mtu yeyote.....oh hello! Kuna wakati unazungumza na watu unaofahamiana nao(wewe unawaita marafiki) na unakutana na suala la maadui......kwamba wanawazungumzia "maadui zao" na jinsi gani wanawachukia halafu unajiuliza imekuaje mpaka hawa watu wanakuwa na maadui? Adui yako anaweza kuwa mtu yeyote kuanzia nduguyo wa damu mpaka yule uliewahi kuchangia nae mwili lakini sasa ni HISTORIA iliyofutika . Sababu za hawa majamaa kuwa maadui zinayofautiana lakini chanzo mara zote (nidhaniavyo mimi) ni ukaribu wao kwako. Ndugu: Unajua Ndugu wa damu mnapokuwa watu wazima mnabadilika (mnakuwa) na ule ukaribu wenu hupungua kutokana na mmoja wenu kuishi maisha tofauti na  (mume au mke) wake. Baadhi ya ndugu huwa bitter wakidhani kuwa huwajali tena na badala yale unajali zaidi mkeo/mumeo na "familia yake".....ni kweli halafu sio kweli kwa kisingizio cha  utahama kwenu na kumfuata mwenza wako. Jam