Tuesday, 15 December 2015

Hii ndio sababu ya mawifi/Mama wake kutuchukia?


Usinielewe vibaya, mie pia ni Wifi "mkubwa", lakini  tofauti ni...sio  kwamba nawachukia(hawajawahi kunikosea) au nawapenda(sijawahi kuishi nao).....nawachukulia kama walivyo na kuwaheshimu kama wanavyoniheshimu.

Kamwe sijawahi/siwezi kujaji lolote kuhusu wao kwasababu siwajui kama ambavyo Kaka zangu wanawajua Wake zao. Sijawahi kuhoji kwenye  kufanana kwao na watoto wao. Huwa nasema tu mnawatoto wazuri, wapwa wangu wanapendeza n.k. Ikiwa Kaka zangu hawakuwa Makini na wanalea watoto wa wenzao, hiyo ni issue yao, sio yangu.
Sasa, kuna siku nilikuwa nazungumza na Asali wa Moyo wangu kuhusu mambo ya Kijamii na tukagusia Chuki ya Wanawake kutoka Upande wa Mwanaume, akaniuliza hivi ni kwanini? Nkamwambia mie pia ni Wifi(mwanamke kutoka upande wa Kaka zangu) lakini sina Chuki na wala sifuatilii mambo yao na familia zao!Tukaenda ndani (deep)kidogo, nikagundua kuwa, chuki hii inaweza kusababishwa na moja9au yote) kati ya haya yafuatayo;-

*Mwanamke anajua kuwa yeye ni "powerful" kwenye maisha ya Mwanaume linapokuja suala la Mtoto/Watoto. Ni yeye pekee ndio anajua baba halisi wa Mtoto ni nani! Hofu ikizidi anaanza  kuhisi kutaka kutafuta "ukweli".


*Watoto alionao pengine sio wa Baba ambae sote tunajua ni Baba yake.


Kwahiyo, ikiwa mmoja kati ya Mawifi au Kiongozi(Ma'mkwe) amewahi kufanya kamchezo kachafu na hakuna anaejua ukweli wa "blending family".....hakika hatokuamini wewe. Siku zote atakuwa wa kwanza kuchunguza kucha za mtoto, rangi ya ngozi, nywele, mwendo, kuota meno n.k.
Sasa ikitokea Mumeo ndio "zao" la kamchezo kachafu ka Mama Mkwe basi utajuta hihihihihi.....unafanya DNA na Babu yake(ambae kihalisia si Baba wa mumeo) mtoto anafeli, unafungashiwa virago wewe na mwanao.....Mumeo anakuchukia Milele.
Siku ingine ikitokea Wifi/Mama mkwe anakusumbua bila sababu ya Msingi, ujue issue ni kutokuamini mtoto/watoto wako ni matunda ya Kaka/Mwana wao...... hakuna kulia na kwenda kushtaki kwa Mumeo. Mwambie  hayo mawili niliyokutajia hapo juu kwa namna yako lakini kwa upole na heshima. Utaona atakavyo kuwa Mdogo au Atakavyokuja juu na "umenikosea heshima" huku analia au kutaka kukuvamia......hapo ujue Umeshinda.
Mf: Wifi/Mama naomba tuongee kama wanawake. Mimi na wewe tunajua kuwa ni sisi pekee ambao tunajua Siri ya Baba wa watoto wetu, sasa kama ilitokea ulitereza na unajua mmoja kati ya wanao baba yake sio Kaka/Ba'mkwe kama tujuavyo, haina maana kuwa na mimi nimefanya hivyo au nitafanya hivyo. Watoto wetu wote ni damu moja(Baba na Mama mmoja).Ahsante kwa kuichagua Blog hii, naheshimu na kuthamini Muda wako hapa.

Babai.

No comments: