Skip to main content

Posts

Showing posts with the label wakwe

Kama Mumeo anakupenda hatoruhusu ufanye haya...

Kutokana na wakati tuliopo ambapo  kuna "informations" nyingi kuhusu nini hasa Mwanamke anapaswa kufanya au kuwa na hivyo kuibua kukanganyana na kudanganyana kuliko wakati wowote ule wa maisha ya Mwanadamu(nimeongeza chumvi, sijui historia ya Mwanamke kabla ya 1900). Hata hivyo bado haiondoi  ukweli kuwa kuwa Mwanamke  mbele ya Wanawake wa kisasa ni Kazi ya Ziada. Mara nyingi sie(wewe na wenzio) wa Kisasa huwa tunaambiana kuwa mwanaume hana haki juu ya mwili wako au uamuzi wako wa nini unataka kufanya na mwili wako(mavazi/Urembo) which it is true  kama ni Mpitaji(boyfriend) lakini ukiwa  kwenye Ndoa/Uhusiano Mwanaume kuonyesha kuwa anajali nini unaweka juu ya mwili wako ni dalili kuwa mwanaume huyo anakupenda na sio kwamba hajiamini au anahofua kuibiwa. Wengi mnadanganyana kuwa Mume(au Mume mtarajiwa) akikukataza usifanye mambo kadhaa ni kuwa anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta kwenye uhusiano wenu. Tunasahau kuwa yeye ni mwanaume na hivyo anajua ni namna gani Wana

Sababu nyingine kwanini tunawachukia Mawifi....

....(Dada wa Wenza wetu) wa sasa au waliopita(Ex), hasa kama mlizaa kabla hamjakutana au  kabla ya kuachana. Kama uliikosa ile ya mwanzo isome hapa . Hello, ipo jambo? Madada huwa na viherehere bin vimbelembele vya kutaka kujua kila kitu, hasa Uhusiano ukiwa bado Mpya tangu kuanza/kuisha. wanaweza kujifanya wapo karibu na wewe na wanakupa support, wanakujua na kukupoenda blablabla. Mawifi hao hao bado ni Shangazi wa Watoto wenu na ni Kaka wa Ex/Current Mumeo,  kwa maana hiyo bado watakuwa karibu na yeyote atakae kuwa na Kaka yao. Hivyo basi kuambiwa/shuhudia mambo mengi/kupewa ripoti kuhusu Mjaza nafasi(mke/Mpenzi mpya) na watoto wake na wakati huohuo wapo karibu na wewe Ex na Watoto wako. Sasa kama wewe ni Ex au Current one mwenye utimamu hakika utaanza kujiweka  mbali na Mawifi kwa sababu chache zifuatazo:- -Hawachelewi kukulaumu kuwa umembadilisha Kaka yao. -Watakuwa wanazungumza na Kaka yao kuhusu Wifi yao wa Sasa na watoto wake na kamwe hawatokuambia(kama wewe ni Ex).

Hii ndio sababu ya mawifi/Mama wake kutuchukia?

Usinielewe vibaya, mie pia ni Wifi "mkubwa", lakini  tofauti ni...sio  kwamba nawachukia(hawajawahi kunikosea) au nawapenda(sijawahi kuishi nao).....nawachukulia kama walivyo na kuwaheshimu kama wanavyoniheshimu. Kamwe sijawahi/siwezi kujaji lolote kuhusu wao kwasababu siwajui kama ambavyo Kaka zangu wanawajua Wake zao. Sijawahi kuhoji kwenye  kufanana kwao na watoto wao. Huwa nasema tu mnawatoto wazuri, wapwa wangu wanapendeza n.k. Ikiwa Kaka zangu hawakuwa Makini na wanalea watoto wa wenzao, hiyo ni issue yao, sio yangu. Sasa, kuna siku nilikuwa nazungumza na Asali wa Moyo wangu kuhusu mambo ya Kijamii na tukagusia Chuki ya Wanawake kutoka Upande wa Mwanaume, akaniuliza hivi ni kwanini? Nkamwambia mie pia ni Wifi(mwanamke kutoka upande wa Kaka zangu) lakini sina Chuki na wala sifuatilii mambo yao na familia zao! Tukaenda ndani (deep)kidogo, nikagundua kuwa, chuki hii inaweza kusababishwa na moja9au yote) kati ya haya yafuatayo;- *Mwanamke anajua kuwa yeye ni