....ndio Asali wa Moyo anaamini hivyo, which is Sad really.....but hey mepata topic!
Wazazi wako walipoamua kuanza familia nadhani ilikuwa ni maana ya Ndoa, kwamba mtafanya Tendo hilo ili kuzaliana. Nia na dhumuni la Tendo la Ngono ni kuzaliana, kama hutaki kuzaa basi tumia Kinga (usiolewe/usioe) si ndio?!!
Kwasisi wa kileo ambao tunabaki Shule kwa muda mrefu, Muda wa kufanya Tendo kwa "haki" (kuzaliana) huwa sio muhimu, lakini pia sio wote tunaweza kuvumilia mpaka muda ufike...hivyo tunaanza Ngono kabla ya Ndoa nakujikinga "Kizungu" Dhidi ya "kuzaliana".
Wazazi kutuzaa sisi ilikuwa uamuzi wao, haikuwa lazima na hakuna aliewalazimisha, sasa kwasababu tu nilizaliwa haina maana na mimi ni lazima nizae. Suala la kuzaa sio rahisi (kwa mwanamke ambae ndio anaezaa)kama ambavyo wengi wanafikiria.
Mwili wa Mwanamke ni wa ajabu in a good way, Ukiachilia mbali Athari na Mabadiliko makuu(mengine yanahatarisha uhai) kwa Mwanamke kwa ndani baada ya kuzaa bado hili suala ni nyeti sana kwa wale ambao hawana uwezo wa Kushika Mimba, kukaa na mimba mpaka ifikie mwisho nakujifungua salama au kupata Mwanaume "anaefaa".
Tunaposema kuwa "tumezaliwa ili tuzae" tunakosea kwasababu Kuzaa sio lazima bali ni Uamuzi kwa baadhi na wengine hawawezi/hawana uwezo wa Kuzaa. Imani hii ni wazi kuwa inawapa Presha Wanawake(kama vile tulizonazo hazitoshi).
Ulipokuwa unakuwa Wazazi wako hawakukuandaa ili uje uzae, walikuandaa Kielimu< Kimaisha ili uweze kujitegemea na kuishi kwa furaha na pengine uwasaidie watakapokuwa Wazee. Unaona? Baba (RIP) na Mama yangu walikuwa wakisistiza kuwa hawataki "Wajukuu" hihihihi go figure!
Suala la Uzazi kwa Mwanamke ni Nyeti mno, huwezi kukurupuka tu na kuzna kusema "mwanamke umeumbwa kuzaa", "tumezaliwa ili tuzae".....vipi kama mtu hana uwezo wa kuzaa? Mwache Mwanamke(kama kajaaliwa uwezo huo) afanye uamuzi wa yeye kutaka Kuzaa, Kuzaa sio lazima, tumezaliwa ili kujifunza, tuishi na kufurahia maisha.....hatukuzaliwa ili tuzae.
Ndio! nakusikia unasema "kama wote tukiamua tusizae Dunia si takuwa tupu" well....zaa wewe uijaze Dunia, wengine ama hawana uwezo, hawapo tayari, hawajapata mtu mwema wa kuzaa nao, au simply hawataki kuzaa.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments