Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mwanamke

Hebu tuone Past life yako: Kuachwa/Telekezwa(2)...

Jambo, ni furaha iliyoje kukutana nawe na ahsante kws kuwa nami leo. Naendelea kukumbusha Maisha uliyopitia ulipokua angali mtoto ili kuona jinsi gani yana athiri Maisha yako hasa kwenye Mahusiano na watu wengine. Kuachwa ni jambo ambalo limezoeleka sana kwenye Jamii(hata za Ulaya ya hapa), kwamba utaachwa, utalia weeee kisha utanyamaza halafu Mzazi akirudi hautokumbuka tena(asiporudi tena baada ya miezi 2? Miaka 3?). Imani hiyo hufanya Wazazi wengi kufanya maamuzi yanayo umiza mtoto(hukumbuka ila hawajui ku-express hisia zao) bila kujua(kwa sababu hata wao walifanyiwa hivyo na they turned out just fine hivyo its okay). Kuachwa/Telekezwa na Mzazi kunafananaje? Mama ambae anamnyima mtoto Nyoyo kwasababu nyingine hana tofauti na Baba ambae hajihusishi (hayupo)kwenye maisha ya mtoto.  Mzazi aliefariki wakati kabla  hujazaliwa/angali ukiwa Mdogo....athari ni zilezile. Na je ni Matendo gani yanaashiria kuwa uliachwa/telekezwa na Mama/Baba na umeathiri? 1-Unapenda "attentuon" na ku...

Hebu tuone Past life yako: Kutelekezwa/Achwa...

Umekuwa na mama yako kwa Miezi 9 mpaka 11 kama ulikuwa na bahati, wengine ni miezi 6 na wengine karibu Mwaka(Miezi 12). Ni mtu pekee unaemfahamu, na unahisi kuwa upo salama na unapendwa, sababu Mtu huyu sio tu amehatarisha maisha yake ili kukubeba na kukuleta Duniani. Mtu huyu ataendelea "kuteseka" sababu unataka ule x4 usiku wa manane, ataendelea kukupenda, kukulinda, kukufunza na kukujali.  Hayo yote hutokea kwa Miezi 3 ya mwanzo, baada ya hapo unamuona mtu huyo Nusu siku, kila unapoachwa unalia sana. Siku zinavyozidi kwenda ukaribu wako na mtu huyo unapungua na kilio chako kinapungua. Kitendo cha Mtu huyo ambae sasa unamtambua kama Mama(au Anty, Dada wa Kazi ndio Mama yako) kukutelekeza/kukuacha huwa kinaumiza sana. Sasa umekua na unajitegemea kwenye mambo mengi kama vile kucheza peke yako, kujivisha viatu/nguo nk. Lakini bado ni Mtoto na bado unamuhitaji Mama yako. Jana la leo Mama amekua nyumbani siku zima, unahisi furaha, upendo na kujaaliwa.....Mama anaamua kutaka kuto...

Social Media, kama ilivyo kwa Dini ni chanzo cha Ndoa/Uhusiano wako kuyumba.

Jambo! Siku kadhaa niliuliza "kiutani" kuwa Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume  kwa Vijana(chini ya Miaka 60)Nchini Tanzania au pengine Afrika linasababishwa na nini? Wawili watatu walidai kuwa Vijana siku hizi wanapiga Mkono(kujichua) kupitiliza, binafsi nilidhani kuwa ni Mawazo kutokana na Ukosefu wa Ajira(Kipato). Hivi majuzi nikakutana na Majadiliano ya Vijana (huku niliko) wakijadili ni namna gani Instagram inawafanya washindwe kuwa watendaji wazuri Kitandani. Sio tu kwamba hawawezi ku-perform bali pia wakifanikiwa kuinuka basi mwenzo huwa mreeeefu na hawafikii mwisho. Kwa kawaida(kiuzoefu) Mzunguuko wa kwanza unaenda kwa Dakika 45 bila Mwanamke kuhisi kuchoka na bila kubadilisha Mikao(unabadili movements za Kiuno/Nyonga), na hii ni kwa Mwanamke mwenye uwezo wa "kukojoa" zaidi ya  mara moja ndani ya Mzunguuko Mmoja(Hisabati nazo zinanifuata kila mahali...I don't like them huh!). Kumbuka baada ya Mwanamke(wa kawaida, sio sie special wa Goli 3 p...

Mpenzi akuone uKizaa vs uKinya.....

Kuna mambo mengine bana ni too personal. Binafsi bora  Asali wa Moyo anione nikizaa(done twice) kuliko anione nikiwa Nashundi. Hii ni Topic ambayo hufanya baadhi ya watu wadhani kuwa hawapendwi vya kutosha. Kwamba kama unapenda mwenzio basi usione aibu Kupumua au Kutoa Haja Kubwa mbele yake. Kama nilivyosema hapo awali kuwa Mie binafsi naamini kuwa Kupumua au kutoa Haja Kubwa ni tendo la "usiri" na ni "personal"......kwasababu tu unaniingilia Kimwili na kuniona Mtupu kila siku, haina maana una "Haki ya Msingi" kuniona nikinya au kusikia nikijamba au hata kuvuta harufu ya Ushuzi wangu nikiwa Macho na nina fahamu zangu kamili(kujamba wakati umelala haihesabiki). Miaka yote niliyoishi na Mume wangu sijawahi Kujamba mbele yake....achilia mbali kujisaidia Haja kubwa akiwa anaoga au anafanya jambo Bafuni. Inawezekana na Makuzi/Malezi ambayo labda Kisaikolojia yamefanya nishindwe kufanya tendo la Kujamba mbele ya watu. Kwetu tulifunzwa kuwa ukitaka ...

Tumezaliwa ili tuzae....

....ndio Asali wa Moyo anaamini hivyo, which is Sad really.....but hey mepata topic! Wazazi wako walipoamua kuanza familia nadhani ilikuwa ni maana ya Ndoa, kwamba mtafanya Tendo hilo ili kuzaliana. Nia na dhumuni la Tendo la Ngono ni kuzaliana, kama hutaki kuzaa basi tumia Kinga (usiolewe/usioe) si ndio?!! Kwasisi wa kileo ambao tunabaki Shule kwa muda mrefu, Muda wa kufanya Tendo kwa "haki" (kuzaliana) huwa  sio muhimu, lakini pia sio wote tunaweza kuvumilia mpaka muda ufike...hivyo tunaanza Ngono kabla ya Ndoa nakujikinga "Kizungu" Dhidi ya "kuzaliana". Wazazi kutuzaa sisi ilikuwa uamuzi wao, haikuwa lazima na hakuna aliewalazimisha, sasa kwasababu tu nilizaliwa haina maana na mimi ni lazima nizae. Suala la kuzaa sio rahisi (kwa mwanamke ambae ndio anaezaa)kama ambavyo wengi wanafikiria. Mwili wa Mwanamke ni wa ajabu in a good way, Ukiachilia mbali Athari na Mabadiliko makuu(mengine yanahatarisha uhai) kwa Mwanamke kwa ndani baad...

Mke anafanyiwa mapenzi, sio the other way around!

Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!! Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie. Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi  kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine  nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini  na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye! Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaan...

Siri ya Mtoto wa Kwanza, Kati na Mwisho....

Inawezekana Ndugu zako wanaokufuata au uliowakuta(inategemea umezaliwa wa ngapi) sio Damu  moja kwamba  baba na mama yenu ni mmoja. Umewahi kujiuliza kwanini mtu anaendelea kuzaa na mume/mke ambae anamtenda(tereza nje)? au Utakuta Ndoa inamatatizo lakini wanazaa tu kila mwaka....haikuhusu lakini kama Binaadam kiasilia hatuishi Kudadisi na Kujaji. Kiasili Watoto tunadhania kuwa Mama zetu ni "Malaika" lakini bwana mwanamke akiamua kushenzika anakuwa Mshenzi zaidi ya Shetwani, tofauti ni kwamba Wanawake ni wazuri kwenye kuficha siri zao. Akitaka usijue Baba yako ni nani basi hutokaa umjue......akikuaminisha kuwa fulani ni Baba yako basi itakuwa hivyo(ukidai DNA unapewa Radhi hihihihihi). Mtoto wa Kwanza: Binti yupo na anaempenda lakini Wazazi hawamtaki Jamaa aoe.....wanataka aolewe na mtu wao. Binti anaolewa na mimba yake bila muoaji kujua. Pia Binti anaweza kuwa anaendelea na ampendae ili azae nae batoto atakaowapenda kama baba yao, kuliko kuzaa na limtu ...