Jambo, ni furaha iliyoje kukutana nawe na ahsante kws kuwa nami leo.
Naendelea kukumbusha Maisha uliyopitia ulipokua angali mtoto ili kuona jinsi gani yana athiri Maisha yako hasa kwenye Mahusiano na watu wengine.
Kuachwa ni jambo ambalo limezoeleka sana kwenye Jamii(hata za Ulaya ya hapa), kwamba utaachwa, utalia weeee kisha utanyamaza halafu Mzazi akirudi hautokumbuka tena(asiporudi tena baada ya miezi 2? Miaka 3?).
Imani hiyo hufanya Wazazi wengi kufanya maamuzi yanayo umiza mtoto(hukumbuka ila hawajui ku-express hisia zao) bila kujua(kwa sababu hata wao walifanyiwa hivyo na they turned out just fine hivyo its okay).
Kuachwa/Telekezwa na Mzazi kunafananaje?
Mama ambae anamnyima mtoto Nyoyo kwasababu nyingine hana tofauti na Baba ambae hajihusishi (hayupo)kwenye maisha ya mtoto.
Mzazi aliefariki wakati kabla hujazaliwa/angali ukiwa Mdogo....athari ni zilezile.
Na je ni Matendo gani yanaashiria kuwa uliachwa/telekezwa na Mama/Baba na umeathiri?
1-Unapenda "attentuon" na kuhakikishiwa/kubalika na jinsia ya mzazi aliekuacha.
2-Huoni shida kuzaa na mtu kisha kutoweka(kutojihusisha na maisha yake).
3-Ni kawaida kujiingiza kwenye Mahusiano/Ndoa za watu.
4- Hujithamini na unapata shida kujikubali.
5-Unaogopa kuachwa na mpenzi hivyo unakataa/ogopa "commitment".
6-Unadharau/chukia jinsia ya Mzazi aliekutelekeza.
7-Unafanya kazi kupita kiasi.
8-Unapenda/furahi kuonewa huruma ama kusifiwa au vyote.
9-Unapata shida kuomba msamaha au kuonyesha shukrani.
10-Huna hali/uhitaji wa kujali hisia za watu wengine(usipokuwa pale tu inapokufaidisha).
11-Mwepesi kujielezea/simulia mambo yako binafsi kwa yeyote mwenye kuonyesha anajali/sikiliza.
12-Unapenda kujipendekeza/tetea tabia mbaya za Jinsia ya Mzazi aliekuacha ili uonekane "special".
13-Unakuwa Mshindani mbaya, kwamba Unahisi Chuki/kushindwa ukiona mtu kafanikiwa kwenye jambo lolote.
Je, unafanya nini ili kuondokana na athari hizo?
Ni kusema yaliyoujaza Moyo kwa Mzazi aliekuacha(kama bado yu Hai au kaenda), kujitahidi kubadilika kwa Msaada wa Kitaalam, Ndugu, jamaa na Marafiki wenye upendo wa kweli kwako na ambao hawaogopi kukuambia ukweli/kosoa.
Kila la kheri.
Comments