Skip to main content

Posts

Showing posts with the label msichana

Hebu tuone Past life yako: Kuachwa/Telekezwa(2)...

Jambo, ni furaha iliyoje kukutana nawe na ahsante kws kuwa nami leo. Naendelea kukumbusha Maisha uliyopitia ulipokua angali mtoto ili kuona jinsi gani yana athiri Maisha yako hasa kwenye Mahusiano na watu wengine. Kuachwa ni jambo ambalo limezoeleka sana kwenye Jamii(hata za Ulaya ya hapa), kwamba utaachwa, utalia weeee kisha utanyamaza halafu Mzazi akirudi hautokumbuka tena(asiporudi tena baada ya miezi 2? Miaka 3?). Imani hiyo hufanya Wazazi wengi kufanya maamuzi yanayo umiza mtoto(hukumbuka ila hawajui ku-express hisia zao) bila kujua(kwa sababu hata wao walifanyiwa hivyo na they turned out just fine hivyo its okay). Kuachwa/Telekezwa na Mzazi kunafananaje? Mama ambae anamnyima mtoto Nyoyo kwasababu nyingine hana tofauti na Baba ambae hajihusishi (hayupo)kwenye maisha ya mtoto.  Mzazi aliefariki wakati kabla  hujazaliwa/angali ukiwa Mdogo....athari ni zilezile. Na je ni Matendo gani yanaashiria kuwa uliachwa/telekezwa na Mama/Baba na umeathiri? 1-Unapenda "attentuon" na ku

Mtoto wa Kiume vs Wa Kike....

....wanatofautiana kwenye kila kitu, kuanzia utungwaji wa Mimba zao mpaka wepesi wa malezi, Ulaji wao na bila kusahau Ughali na Urahisi wa Mavazi. Kwa uzoefu wangu so far Mtoto wa Kiume ni rahisi ku-deal nae kuliko wa Kike(labda ni Homono).....Lakini Mtoto wa Kiume ni Ghali kuliko wa Kike linapokuja suala la Toys na Mvazi. Tukiacha tofauti hizo na nyingine ambazo wewe unauzoefu nazo, bado wote ni Watoto na wanahitaji Upendo, Mafunzo, Elimu, Ulizi etc sawa sawa. Natambua kwa Wazazi wetu ilikuwa tofauti, kwamba Msichana alikuwa akilindwa zaidi kuliko Mvulana. Baadhi ya Wazazi wa sasa bado wanaendelea na "Kasumba" hiyo ambayo mie nahisi kuwa imepitwa na wakati(inaharibu upande mmoja). Ni imani iliyojengwa miongoni mwetu kuwa Mtoto wa Kike ni "dhaifu" na hivyo ni rahisi kushawishika na kufanyiwa mabaya/kuharibiwa kuliko Mtoto wa Kiume.  Hii inafanya kuongeza "ulinzi" na Elimu juu ya "Watu wabaya" dhidi yao. Inasahaulika  kuwa huyu