Soma Mosi na Pili hapa....
Tatu, Mtoto anamuhitaji Mama yake full time kwa Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake baada ya hapo PT sio mbaya.
Malezi ni Kazi kama kazi nyingine na inachosha Akili na Mwili, tofauti ni kwamba hakuna Likizo na huwezi kuacha/badilisha na pia kwa Tz Mke (Mama wa Mtoto) huwa halipwi na hiyo inafanya kuwa "Kazi" hiyo kuonekana kuwa ni rahisi.
Mkeo anapoamua au mnapokubaliana kuwa yeye abaki Nyumbani kulea watoto ni jambo zuri na la kuheshimika kwa Ulimwengu wa sasa.
Mkeo akigoma kufanya Kazi ya Kulea na kuamua kwenda kufanya kazi/biashara nje ya nyumbani ni wazi kuwa mtahitaji "Mlezi" wa watoto wenu wa hapo nyumbani na yule wa "shule", na atalipwa kwa "rate" nzuri tu kulingana na Kipato/aina ya Maisha mnayoendesha.
Wengi kwenye Mitandao wamelichukulia suala la Amina na Kiba kwa kuangalia Kona ya maisha waliyonayo wao kwa sasa, na sio Maisha ya Star Mkubwa mwenye Thamani ya Dollar Millioni 5(11,570,000,000).
Pia imesahaulika kuwa Kesi imefunguliwa Nchini Kenya ambako ndiko walipofungoa Ndoa(kwa mujibu wa Magazeti ya Kenya). Huko kwa Majirani wapo mbele kiasi linapokuja suala la kufuata Sheria.
Binafsi sipendi watu wanaokimbilia Talaka kabla ya kujaribu/jitahidi kubadilika na kuokoa Ndoa yao. Lakini kila Ndoa huwa na Mipaka ya kujiwekea na ile ya Imani(wanayoifuata wahusika).
Usipoheshimu Mipaka ya mwenzio na kuivuka, Ndoa haiwezi kupona/simama tena.
Comments