Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kenya

Amina wa Ali Kiba adai Talaka Mahakamani na Kiba(2)....

Soma Mosi na Pili hapa .... Tatu, Mtoto anamuhitaji Mama yake full time kwa Miaka 5 ya mwanzo ya Maisha yake baada ya hapo PT sio mbaya. Malezi ni Kazi  kama kazi nyingine na inachosha Akili na Mwili, tofauti ni kwamba hakuna Likizo na huwezi kuacha/badilisha na pia kwa  Tz Mke (Mama wa Mtoto) huwa halipwi na hiyo inafanya kuwa "Kazi" hiyo kuonekana kuwa ni rahisi. Mkeo anapoamua au mnapokubaliana kuwa yeye abaki Nyumbani kulea watoto ni jambo zuri na la kuheshimika kwa Ulimwengu wa sasa. Mkeo akigoma kufanya Kazi ya Kulea na kuamua kwenda kufanya kazi/biashara nje ya nyumbani ni wazi kuwa mtahitaji "Mlezi" wa watoto wenu wa hapo nyumbani na yule wa "shule", na atalipwa kwa "rate" nzuri tu kulingana na Kipato/aina ya Maisha mnayoendesha. Wengi kwenye Mitandao wamelichukulia suala la Amina na Kiba kwa kuangalia Kona ya maisha waliyonayo wao kwa sasa, na sio Maisha ya Star Mkubwa mwenye Thamani ya Dollar  Millioni 5(11,570,000,000). Pi

Kurekebisha/Komesha Tabia online, inawezekana?

Habariyo! Mengi kama sio karibu yote siku hizi yanawezekana Online, lakini kurekebisha Tabia ya mtu au watu Online? mie Mshamba hivyo sidhani kama inawezekama. Huwezi kumfunza mtu tabia njema ikiwa hakufunzwa hivyo na Wazazi/Walezi wake! Utakachokifanya ni kufanya watu wakuogope au Waogope kuwa karibu na wewe (unless ufiche Utambulisho wako). Inaaminika kuwa ni vigumu sana kwa Mtu kubadilika Kitabia akisha vuka Umri wa Miaka 25, atajaribu "kuacha" tabia yake ikiwa tu  kaamua iwe hivyo na kuna mtu wa karibu yake pembeni anamsaidia, lakini "msaidizi" akiondoka maishani mwake basi Mhusika hurudia tabia yake/zake Mbaya. Vilevile, ikiwa Mhusika mwenye Tabia mbaya amejenga Familia na Mtu ambae ana-support au kuelewa au samehe tabia yake mbaya, basi ugumu wa mhusika kubadilika huongezeka, kwasababu ana "support system"kutoka kwa Mke/Mumewe ambae ni Muhimu kuliko watu wengine wote wa online included. Kitambo hivi, kuna jamaa Walipatw