Habariyo!
Mengi kama sio karibu yote siku hizi yanawezekana Online, lakini kurekebisha Tabia ya mtu au watu Online? mie Mshamba hivyo sidhani kama inawezekama. Huwezi kumfunza mtu tabia njema ikiwa hakufunzwa hivyo na Wazazi/Walezi wake! Utakachokifanya ni kufanya watu wakuogope au Waogope kuwa karibu na wewe (unless ufiche Utambulisho wako).
Inaaminika kuwa ni vigumu sana kwa Mtu kubadilika Kitabia akisha vuka Umri wa Miaka 25, atajaribu "kuacha" tabia yake ikiwa tu kaamua iwe hivyo na kuna mtu wa karibu yake pembeni anamsaidia, lakini "msaidizi" akiondoka maishani mwake basi Mhusika hurudia tabia yake/zake Mbaya.
Vilevile, ikiwa Mhusika mwenye Tabia mbaya amejenga Familia na Mtu ambae ana-support au kuelewa au samehe tabia yake mbaya, basi ugumu wa mhusika kubadilika huongezeka, kwasababu ana "support system"kutoka kwa Mke/Mumewe ambae ni Muhimu kuliko watu wengine wote wa online included.
Kitambo hivi, kuna jamaa Walipatwa na Msiba. Sasa jamaa walikuwa wakiishi kivyao-vyao(hawana habari)na hawakujichanganya na Watz wenzao huko waliko Ughaibuni. Inasemekana walikuwa hawashiriki "Sosho events" za watu soooo walipofikwa na hiyo "life situation". Watu wakaamua kuwafunza "adabu Online".
Mie nilipoambiwa nikawashangaa watoa Adabu. Kwanini mtumie Maumivu ya watu kuwadhalilisha.....sawa nyie ni Watz zaidi yao(Wafiwa wanaishi Kizungu) basi toeni Adabu kiTz, Kijadi. Unakumbuka Utani Msibani? yep watu bado wanafanya haya na tulipofiwa na Mzee(Baba RIP) watani walitutania na kumuigiza marehemu Baba, baadhi unacheka na mengine yanakuongezea Uchungu zaidi.
Watani hutumiwa Misibani kufikisha Ujumbe/Funzo/Tia Adabu "live" uliochanganyikana na Utani, sasa kama alietangulia alikuwa wa kujidai-Pua juu ndio mtajuzwa siku hiyo, Kutokana na Utu Washiriki watakuja Msibai lakini watafanya kwa "utani" vile ambavyo ulikuwa ukifanya kwenye matukio kama hayo kwa wenzako na mwisho kususia "Shughuli" ili kuwafunza Adabu Waliobaki. Baada ya tukuio kupita utaanza kuona Wanafamilia wakianza "kubadilika" na kuanza kushiriki Matukio ya Kimaisha ya Jamii inayowazunguuka.
Hili haliwezi kuhamishiwa Online, unachokifanya Online ni kuiaibisha Familia ya mwenzio kwa kisingizio cha Kufunza tabia. Asilimia 99.9 wahusika hawatosoma/ona na wengi watakaosoma sio wahusika uliowakusudia. Kwa maana nyingine wale uliowakusudia wataendelea na "Uzungu wao" kama kawaida.
Mie binafsi sio Mtu ninaependa Mikusanyiko lakini huwa nashiriki kwenye Matukio ambayo nahisi kuwa ni Muhimu kama vile Msiba au Michango kwa ajili kusaidia Matibabu. Kwenye sherehe-sherehe hunikuti.
Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa ni sawa kabisa kujitenga(kutokuwa mtu wa mikusanyiko) lakini mtu unaemfahamu anapopatwa na Shida ni vema kutafuta muda na kushiriki. Natambua maisha ya Ughaibuni yanabana sana linapokuja suala la Muda(nafasi), Ugumu huongezeka mnapokuwa na Watoto.
Lakini ni muhimu kujigawa, hii ita-sound kizungu pia hihihihihihi tupo Uzunguni babu wee hehehehe. Kama ambavyo tunajigawa kwenye maswala mengine ya kimaisha kama vile bills, shopping....mjigawe, nani atakuwa anawakilisha Familia kwenye "life situation" kwenye jamii inayokuzunguuka iwe ni ya Wabongo wenzako au mchanganyiko.
Wakati mwingine sio rahisi kuwepo "live" kwenye tukio kutokana na Umbali wa Jimbo to Jimbo, Mkoa toMkoa, kwa UK ni Nchi na Nchi, basi tumia Simu eeh, shiriki ki-Digital.
Nashukuru na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments