Habariyo! Mengi kama sio karibu yote siku hizi yanawezekana Online, lakini kurekebisha Tabia ya mtu au watu Online? mie Mshamba hivyo sidhani kama inawezekama. Huwezi kumfunza mtu tabia njema ikiwa hakufunzwa hivyo na Wazazi/Walezi wake! Utakachokifanya ni kufanya watu wakuogope au Waogope kuwa karibu na wewe (unless ufiche Utambulisho wako). Inaaminika kuwa ni vigumu sana kwa Mtu kubadilika Kitabia akisha vuka Umri wa Miaka 25, atajaribu "kuacha" tabia yake ikiwa tu kaamua iwe hivyo na kuna mtu wa karibu yake pembeni anamsaidia, lakini "msaidizi" akiondoka maishani mwake basi Mhusika hurudia tabia yake/zake Mbaya. Vilevile, ikiwa Mhusika mwenye Tabia mbaya amejenga Familia na Mtu ambae ana-support au kuelewa au samehe tabia yake mbaya, basi ugumu wa mhusika kubadilika huongezeka, kwasababu ana "support system"kutoka kwa Mke/Mumewe ambae ni Muhimu kuliko watu wengine wote wa online included. Kitambo hivi, kuna jamaa Walipatw...