Skip to main content

Posts

Showing posts with the label tabia

Jinsi ya kujenga/kuza“character” ya mtoto wako.

Jambo wewe, Kulea Watoto Ughaibuni ambako kuna Kacha tofauti na Kacha tuliokulia nazo inaweza kuwa a bit confused, hasa kama umetoka zako Afrika (bongo as in Tz ikiwepo) na Kacha ya U-marekani mweusi. Unazaa Watoto na hujui uwalee katika kacha gani, nap engine unajiuliza hivi huku ulipo wanao wana kacha yeyote au wafuate kacha ya watu wanaofanana nao(Weusi wenzao aka Black Culture)? Unasahau kuwa kila mweusi wa Ulaya ana kacha yake aliokuzwa nao kulingana kabila lake na wapi anatokea Afrika.     Kwa kifupi nchi kama UK hakuna Black culture (wanalazimisha kuuingiza U-black Amarekan) bali kuna Culture za Afrika na Caribbean ila kwa wale wazazi waliokuja na U-black amerika kutoka Afrika basi huamini kuwa Culture ya Black amerika ndio Black culture Dunia nzima na hivyo kuindeleza. Hizo kacha   zetu za Afrika na Caribbean hazidumishwi na Taifa zaima la UK isipokuwa jamii husika ni kama ambavyo jamii nyingine ya wazungu kutodumisha Kacha zao Kitaifa kwasababu UK ina mataifa mengi hivyo k

Kurekebisha/Komesha Tabia online, inawezekana?

Habariyo! Mengi kama sio karibu yote siku hizi yanawezekana Online, lakini kurekebisha Tabia ya mtu au watu Online? mie Mshamba hivyo sidhani kama inawezekama. Huwezi kumfunza mtu tabia njema ikiwa hakufunzwa hivyo na Wazazi/Walezi wake! Utakachokifanya ni kufanya watu wakuogope au Waogope kuwa karibu na wewe (unless ufiche Utambulisho wako). Inaaminika kuwa ni vigumu sana kwa Mtu kubadilika Kitabia akisha vuka Umri wa Miaka 25, atajaribu "kuacha" tabia yake ikiwa tu  kaamua iwe hivyo na kuna mtu wa karibu yake pembeni anamsaidia, lakini "msaidizi" akiondoka maishani mwake basi Mhusika hurudia tabia yake/zake Mbaya. Vilevile, ikiwa Mhusika mwenye Tabia mbaya amejenga Familia na Mtu ambae ana-support au kuelewa au samehe tabia yake mbaya, basi ugumu wa mhusika kubadilika huongezeka, kwasababu ana "support system"kutoka kwa Mke/Mumewe ambae ni Muhimu kuliko watu wengine wote wa online included. Kitambo hivi, kuna jamaa Walipatw