Jambo wewe,
Kulea Watoto Ughaibuni ambako kuna Kacha tofauti na Kacha tuliokulia nazo inaweza kuwa a bit confused, hasa kama umetoka zako Afrika (bongo as in Tz ikiwepo) na Kacha ya U-marekani mweusi. Unazaa Watoto na hujui uwalee katika kacha gani, nap engine unajiuliza hivi huku ulipo wanao wana kacha yeyote au wafuate kacha ya watu wanaofanana nao(Weusi wenzao aka Black Culture)? Unasahau kuwa kila mweusi wa Ulaya ana kacha yake aliokuzwa nao kulingana kabila lake na wapi anatokea Afrika.
Sasa, kulea Watoto kwakufuata mkondo wa ulioishi wewe kwa kufuata Kacha yako bila wao kuishi kwenye mazingira husika binafsi naona sio sahihi, kulea watoto katika miongozo ya tabia njema na kufuata maadili/values za Dini(sio za makanisa ya kisasa ones) ni muhimu. Pamoja na hayo pia ni vema kama wazazi kuweka nguvu ya ziada kwenye kujenga “character” zao….na hii ndio topic ya leo.
Unajengaje
character/tabia ya Watoto wako ili wakawe na mwanzo mwema out there?
Kwa kawaida
unaanza mapema sana, kabla mtoto hajafikisha miaka 3, unamfunza kusalimia, kuomba,
kusema ahsante na kusema samahani. Jinsi anavyokuwa unaendelea kumfunza na
kurudia mara zote unahisi kuwa ni muhimu…unajua
jinsi inavyokua.
-Majukumu:
Mfunze na msaidie ajue majukumu yake na namna ya kuyatimiza, mf kwa kuanzia ni
lazima aoge, alainishe ngozi, achane/tengeneze nywele, avae vizuri(we
presentable), asafike chumba chake n.k.(zingatia umri).
-Kukubali makosa
na kuomba radhi (ndio Accountability?): Hii ndani kwetu imeanza mapema sana
kwasababu tulichagua kuwa Watoto humu ndani wana haki kama wanadamu na kwamba
wao sio bidhaa zetu, kwamba hata tukikosea kama wazazi bado tupo sahihi na
hakuna kuomba radhi. Mtoto akija kwako na kulalamika kuwa umemkosea na unajua
kabisa umemkosea, omba radhi. Na mfunze mwanao hivyo, rahisi ikiwa ana wadogo
zake.
-Ushirikiano:
Kufanya kazi kama timu ili kufikia lengo, iwe shuleni au nyumbani katika kusafisha nyumba,
kuandaa/tenga meza/mkeka/jamvi kwa ajili
ya chakula, kucheza na wakati mwingine kusaidia kazi nyingine pale inapobidi.
-Shukurani: Ajue
kushukuru sio tu kwavile mnamnunulia
vitu atakavyo, bali pia kwa sababu kaamka akiwa salama, ana afya njema ana
wazazi wote wawili na wadogo/wakubwa wake ambao wanampenda na vitu vingine
alivyo navyo kwa wakati husika.
Msimamo: Asimamie
anacho kijua na kuamini (inategemea na Imani yenu ya Dini na mambo mengine
mnayomfunza kulingana na uzoefu wenu)ambacho ni kizuri/chema sio kwake tu bali
kwa jamii nzima inayokuzunguka.
-Utu: Mfunze
mwanao aweke mbele utu, kwa kukumbuka watu wengine katika maombi na atoe Sadaka kwa kusaidia wengine wenye uhitaji(hii inafunzwa zaidi Kanisani)awe mwenye huruma lakini asivuke mipaka.
-Kujizuia:Ajue
kujizuia linapokuja suala la kukabiliana hasira, frustrations hii hujitokeza pale
unapomfunza mf Hisabati halafu hapatii, kila akirudia bado anakosea….hapa ndio
pa kuanzia kumfunza self-control. Itachukua muda lakini ataweza. Hii pia
itamsaidia kujua how to pale wewe mzazi nay eye mkifikia kwenye suala la kukabiliana
na Hisia mbali mbali.
Sote tunajua
Maisha ni magumu, tujitahidi kuwasaidia Watoto wetu ili wawe na Maisha mepezi
kiasi sio kiuchumu tu, bali kitabia pia.
Pole kwa kusoma neno “Kacha” mara 820 😐.
Comments