Skip to main content

Talaka ya Amina kwa Ali Kiba...

Mimi na wewe hatujui kwa Undani ni kitu gani hasa kilichopelekea wawili hao kufunga Ndoa 2018.


Lakini kutokana na Maelezo ya Amina kwenye Hati ya Madai tunajua kuwa Kiba alikuwa Mtesi/Mnyanyasaji kwa Mkewe (Kiakili, Kimwili, na Kisaikolojia)baada ya Miezi 6 ya Ndoa.



Kwa maelezo hayo inaonyesha kuwa Amina hakuwa "kipenzi" cha Familia ya Mumewe na hivyo kuhisi kuwa mahali walipo watu hao sio Salama kwake na kwa Watoto na hivyo kurudi kwao Mombasa*.




Pia Amina ameongeza kuwa Mumewe(Kiba)ni Muasherati na hakuiheshimu yeye(Amina) wala Ndoa yao(alimdhalili adharani).



Amina amedai kiasi cha Laki mbili kwa mwezi(Ksh) kwa ajili ya Matunzo yake na watoto. Madai ambayo yamesababisha Watanzania wa Twita kuhoji...


Tu(na)jigunza nini kwenye tukio hilo.

Moja, Kwa Msanii mkubwa kama Ali Kiba ambae ana Thamani ya Dollar Millioni 5(568,500,000Ksh) Laki mbili kwa mwezi kwa mahitaji ya Mtoto sio pesa nyingi, pengine haitoshi tukiongeza Ulinzi, Usafiri na Bima ya Afya. 


Unalipa Matunzo kwa watoto na Mkeo kulingana na Umri wa Ndoa na Makadirio ya  Kipato kwa miaka kadhaa mbele(inaweza kupanda/kushuka). Hilo Moja.



Pili, Mwanamke kabla ya kufunga Ndoa na mtu unapaswa kujua shughuli zake na "kacha"  ya shughuli hizo(sio kuangalia pesa na kuipenda lifestyle tu). Mf; Kiba ni Msanii, ana wapenzi na WAPENZI  wa Sanaa yake. 



Simtetei lakini unapokubali kuolewa na mtu anaefanya Kazi zake Usiku, Mashabiki wake 85% ni Wanawake na kama ilivyo kwenye Ndoa yeyote anapambana na majaribu mengi(kama sie mama wa nyumbani wa huku na handymen), unakuwa umejitolea Mhanga(lazma uwe na roho ngumu). Pili.
 

Hivi ni kwanini Handymen wa Nchi hii ni Wasupu? Turudi kwa Amina na Ali.


Inaendelea...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao