Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!!
Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie.
Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye!
Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaani wanasubiri kupakuliwa(sio wote). Mbaya zaidi kuna hata maneno kwenye Nyimbo zilizoimbwa na Wanawake zinakubaliana na kusisitiza kuwa Mwanamke "mambo" au "kujituma" au "kujua wajibu wako" Kitandani.
Lakini kihalisia Mwanaume ndio anapaswa kumfanyia Mapenzi Mkewe/Mwanamke wake, sio tu kwasababu "kuneng'enuka" kwetu kunahitaji akili kutulia (hatuna mawazo wala hofu) bali pia mwanamke anahitaji kuhisi kuwa anapendwa na kutakwa na wewe(mwanaume) ili afurahie Safari ya Kuneng'enuka.
Kwenu ninyi wanaume Ngono ni Ngono tu, unachohitaji ni mtu kukubali kufanya.....mfano Mwaname akisema "nataka unifanye" unakuwa tayari....au unaeza kuona upindo wa Chupi ukawa umefika(hihihihihi). Wanawake pia huwa tayari ila sio kila siku(inategemea na Mahesabu ya Mzunguuko).
Kuna siku za Mzunguuko unahitaji kupendwa zaidi ya siku nyingine, kuna siku unahitaji kuguswa Bega au kiuno na ukawa "tayari", siku nyingine unahitaji kupendwa na kufanya Malkia kwa Dakika 45(duh hizi nyingi.....tufanye Dakika 20 hivi).
Siku nikipata Muda(nikikumbuka that is) nitakuletea "hisia" za Mwanamke kulingana na Mzunguuko wake wa Hedhi (siku 28 ndio nina uzoefu nayo) ili ikusaidie kujua kuwa Leo akitaka kuwa in control na ku-make love to you haina maana itakuwa hivyo siku zote za Mwezi. Inaeza tokea mara moja au Mbili tu.....usizoee!
Ili uwe Mfalme ni wazi kuwa unahita Malkia.......ila kumbuka Malkia hawezi kuwepo bila ya kuwa na Mfalme kwanza. Mwanamke kwanza!
Naheshimu na kuthamini Muda wako wapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments