...pengine hujawahi kuambiwa kuhusu hili la "kijinyama", "Kijingozi" lakini lipo na huwatokea wanawake wengi tu, tatizo ni kuwa wengi hawapendi kulizungumzia.....Uanake ni zaidi ya Makeup, Matiti na Kuvaa Magauni na Blauzi.
Umewahi kujiswafi na ukakutana na kitu cha ajabu ukaanza kuogopa n a kudhani Kizazi kimetoka(hahahaha) au Mimba imeharibika bilakujua kama ulikuwa nayo au ukadhani Umelogwa ili upate Hedhi ya Manyama badala ya Damu?
Mara nyingi hii hutokea mara tu baada ya Kumaliza Hedhi na kufanya Mapenzi, au pengine umefanya Mapenzi na Mwenza akaenda "mbali" na baada ya kumaliza ukaona Damu na baada ya kujiswafi ukatoa "kijinyama" ambacho hakiterezi kama Ute Mzito au Damu nzito......usiogope hasa kama Umeruka Hedhi.
![]() |
Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke |
Ukuta wa Mji wa Uzazi(Uterus/Womb) hujijenga kila baada ya siku 23 na baada ya hapo hung'oka na kuteremka sambamba na Damu pale unapokuwa Hedhini....sasa ikiwa umepitiliza au kuruka Hedhi moja au mbili, Ukuta ule ambao ni ngozi/kijinyama huwa mnene zaidi na hivyo kugoma/kwamba wakati una-Hedhi-ka kile kijingozi hakiteremki moja kwa moja Ukeni(Vagina) na matokeo yake hubaki ndani pale pembeni mwa Mlango wa Uzazi (Cervix).
Wakati mwingine huwa imeng'ang'ania na hivyo baada ya Uume kuingia na kufanya Uume ufanyavyo "best" kile kijinyama hujiachia na hivyo kuwa tayari kutoka kwa msaada wa kidole chako na Maji. Kama huna utaratibu wa Kujiswafi Ukeni ni wazi kuwa kitakaa huko na baadae kusababisha maambukizo au kutoa "ute" wa rangi ya ajabu (kahawia) na harufu mbaya.
Huenda hujawahi kutwa na hili hasa kama Mzunguuko wako sio wa Kuruka(unaenda Kila Mwezi) na haujawahi Kuzaa na Kunyonyesha. Kama nilivyogusia hapo juu, kuwa kila baada ya Hedhi Ukuta wa Mji wa Mimba hujijenga na hung'oka baada ya muda ikiwa hakuna Yai lililorutubishwa na "ukuta" huo kuteremka sambamba na Damu yako ya Hedhi(Mie sio Daktari usiniulize Maswali).
Sasa ukizaa na ukawa unanyonyesha mara nyingi unapoteza Hedhi(hupati Hedhi mpaka umalize Kunyonyesha sio!), mpaka Hedhi bin Homono vinakuja kutulia baada ya kunyonyesha ni wazi kuwa utakuwa unaruka-ruka na hivyo "ukuta" wa Mji wa Uzazi wako kuwa Mnene na hivyo kutoka kama nilivyoelezea hapo awali.
Pamoja na kuwa nimekutoa hofu bado ni Muhimu kwako kwenda Kumuona Daktari wa Magonjwa ya Kike na umuelezee hali halisi, jitahidi kuweka kumbukumbu ya Tarehe na aina/ukubwa/udogo wa "kijinyama" hicho ili Daktari aweze kukuelewa zaidi nahivyo kufanyiwa Vipimo yakinifu kuangalia kama Mfumo wako wa Uzazi upo na afya njema.
Naheshimu na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments