....ndio mnaita "Fussy eater" eti? Baadhi ya Watoto huanza mapema(au wazazi wao wanaamua kuwa watoto wao ni fussy kama sifa) katika hali halisi ni Uchovu unaopelekea kutokuwa na utararibu wa "kula" na attention ya kutosha kwenye kula kwa mtoto husika! Kamwe sitokufunza namna ya kule mwanao, isipokuwa nitachangia uzoefu wangu ili kwa namna moja ujione kuwa haupo peke yako na hivyo kupata nafuu na pengine kuchukua "tips" na kujaribu ili mwanao apate virutubisho vyote Asilia ambavyo ni Muhimu kwa Ukuaji wake. Mwanangu wa Kwanza(Babuu) alianza kula Vizuri sana akiwa na Miezi Sita, alipofikisha Mwaka na Miezi 3(Miezi 15) akacha kunyonya mwenyewe(bila kuachishwa). Babuu alikuwa anakula kila aina ya Chakula unachompatia. Alipofikisha Miaka 2 hali ikabadilika, akaanza kukataa Nyama na Samaki which was Okay kwasababu alikuwa akila Mayai vema. Alipofika Miaka 2 na Nusu akawa anakula Viazi tu.....tena viwe vimepondwa(mashed). Ukichanganya Mchuzi au Mbog