Skip to main content

Mtoto "anaechagua" Vyakula....

....ndio mnaita "Fussy eater" eti?

Baadhi ya Watoto huanza mapema(au wazazi wao wanaamua kuwa watoto wao ni fussy kama sifa) katika hali halisi ni Uchovu unaopelekea kutokuwa na utararibu wa "kula" na attention ya kutosha kwenye kula kwa mtoto husika!


Kamwe sitokufunza namna ya kule mwanao, isipokuwa nitachangia uzoefu wangu ili kwa namna moja ujione kuwa haupo peke yako na hivyo kupata nafuu na pengine kuchukua "tips" na kujaribu ili mwanao apate virutubisho vyote Asilia ambavyo ni Muhimu kwa Ukuaji wake.



Mwanangu wa Kwanza(Babuu) alianza kula Vizuri sana akiwa na Miezi Sita, alipofikisha Mwaka na Miezi 3(Miezi 15) akacha kunyonya mwenyewe(bila kuachishwa). Babuu alikuwa anakula kila aina ya Chakula unachompatia. Alipofikisha Miaka 2 hali ikabadilika, akaanza kukataa Nyama na Samaki which was Okay kwasababu alikuwa akila Mayai vema. Alipofika Miaka 2 na Nusu akawa anakula Viazi tu.....tena viwe vimepondwa(mashed).




Ukichanganya Mchuzi au Mboga-mboga kwenye  Viazi vyake "mashed", anasema "sipendi harufu" so anagoma kula na kuomba Maziwa.....then unampa Maziwa wakati anasubiri umtengenezee Viazi vingine bila "shombo". Mimi kama mimi, nikabeba Mwanangu huyoo mpaka kwa Daktari wake nakushtaki(kuelezea), Daktari akasema so long anakula Viazi, Mayai na Maziwa ni okay, ila niongeze matunda between meals! Hapana, sikufanikiwa.....tukarudi na kubaki kwenye  Viazi vya kuponda/Saga.




Wataalamu wanasema kuwa ni kawaida kwa Mtoto kuwa mchaguzi linapokuja suala la kula na kwamba ni sehemu ya Ukuaji. Wao wanatoa "Tips" kwa ujumla ili wazazi wenye watoto fussy tuzijaribu....napenda kukuhakikishia kuwa  nimejaribu zote na hakuna hata  moja iliyonisaidia.




Nikagundua kuwa Mama (au anaekutunzia mwanao unapokuwa Kazini) unakuwa na shughuli nyingi na zile Homono huwa hazijirudi haraka kwa baadhi yetu na hivyo kuna wakati unajisahau na badala ya kumpa mtoto chakula unampa maziwa kwanza ili aponze  njaa kisha ndio chakula(hapa lazma akatae), kosa ni kuwa anaponyonya njaa inakwisha, watoto sio kama sisi watu wazima. Kwamba njaa ikuma unakunywa Chai na kipande cha Mkate wakati unasubiri chakula kiive, Maziwa tumboni mwa mtoto wa umri wa Miezi 6 hadi miaka 4  hudumu kwa Masaa2+.



Kumbuka, mtoto bado anajifunza kil akitu kwa mara ya kwanza, sasa usipokuwa na utaratibu unaojirudia utakaomfanya azoee na kuona kuwa ni "kawaida" anachanganyikiwa na kusahau at the same time!



Sasa ile kutokuwa na utaratibu unamchanganya mtoto (kama nilivyosema)na matokeo yake anaanza kuchukia kula(unamlazimisha kula wakati hana njaa), hii haina "mtoto anataka kujitegemea kama Wazungu wanavyosema", hii  ni Mzazi/Mlezi kutokuwa  na utaratibu unaojirudia na wao kula kama Mazoea badala ya kula ili wapate nguvu/wakue(nia ni moja kuwa wale wakue na kujenga mwili ktk mtindo tofauti).



Haikuwa kazi rahisi kumfanya Babuu aanze kula vizuri au niseme kawaida (isipokuwa Nyama), Zifuatazo ni Tips zangu Binafsi ambazo zinaweza kukusaidia  kama Mwanao ni Fussy eater;-


easy way kupata Matunda na Mboga 5 a day

1-Weka utaratibu wa Masaa ya Kula, Mf: Saa 8 Kifungua kinywa, Saa Nne na Nusu Snack, Saa Sita  Mlo wa Mchana , Saa nane na Nusu Snack, na Saa Kumi  na Moja Mlo wa Jioni na Saa Moja jioni Maziwa(husisia ku-relax na hivyo analala haraka)



2-Usizidishe kipimo kwenye "snacks", kumbuka hii ni kupitisha muda kabla ya Chakula, sasa kama umeweka Maziwa/mayai ndio snack basi hakikisha unampatia kidogo ili asishibe.



3-Mpe Choice(kama uchumi unaruhusu na anamika 2+), Utapenda maziwa na vitumbua au Maziwa na Mayai?....anaweza kusema Mziwa tu, mwambie ale kitafunwa kwanza halafu atapata Maziwa.



4-Usimfokee, usimkaripie na wala usimlazimishe kula.....mbembeleze kula, ikiwezekana Mlishe(memlisha Babuu mpaka mwaka jana hihihihihi).....achana na  ile "tukienda kwa watu itakuwa aibu mtoto wa miaka 4 bado namlisha",...pima Wao vs Afya ya Mwanao.



5-Kama kuna shughuli, hakikisha unambebea mwanao chakula chake unachojua anakipenda, ikiwezekana mlishe kabisa kabla hamjatoka.




6-Chagua aina moja ya Mboga ambayo ni "super food" lakini haina Harufu/Radha kali.....mie nilichagua Mchicha na Kale. Changanya Tutunda tamu na laini kama vile Papai, Embe, Zazibu, Ndizi na Moja ya Mboga hizo zikiwa Mbichi(bila shaka ni baada ya kuosha ) halafu changanya Vijiko Viwili Vikubwa cha chakula kwenye Mlo wake wa Mchana au Jioni. Na ikiwa mwanao ni mpenzi wa Mash basi ni nafuu kwako na kwake.




Kumbuka Mwanao ni  tofauti na hakuna kama yeye Duniani, ni an individual/his/her own little person hivyo usimfananishe/linganishe na watoto wengine wa umri wake au wadogo kwake. Muhimu ni kwa Mwanao kupata uzoefu wa radha tofauti tena kama ilivyokuwa mwanzo wakati unaanza kumtambulisha kwenye vyakula ili aache kunyonya, tofauti sasa  ni Mkubwa na anahitaji virutubisho zaidi kwani havipati via Nyoyo yako anymore. Amekuwa so Mashed kila kitu ni muokozi wako kwa sasa.



Inakatisha tamaa, inachosha wakati mwingine.....lakini usikate tamaa. Jaribu Tips zangu.....hata akila vijiko 3 bado mchanganyiko huo utamsaidia ndani na nje ya Mwili.


Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao