....nirahisi kupatwa/kabiliana na mengi kwenye Maisha yako na hivyo kujifunza zaidi, kuliko kujua kila situation ya mtu, achilia mbali watu ambao sio wewe. Niliwahi ku-blog kuhusu tabia ya watu "kujifanya" wanamjua kila mtu au zaidi "celeb" na life situations zao. Hakika hilo linawezekana, lakini ni vema kuweka wazi kuwa unayajua hayo yote kwasababu ya kusoma Gossip Sites/Blogs/TvChanells/Vijiwe/Joints n.k. na sio kwamba unawajua hao watu individually.
Kutokana na Maendeleo ya Kiteknolojia, mawasiliano yamerahisishwa na hivyo baadhi yetu huwa tunapata Majibu/Ushauri wa Maswali/Matatizo yanayotukabili papo kwa hapo. Urahisi huu unafanya wengine kupitiliza kwenye kuchangia "uzoefu" wao kwenye "situations" nyingi kwenye Sosho midia husika na hivyo kukera baadhi.
Mie binafsi nina majibu mengi zaidi kuliko your "normal" Dada, kwasababu pengine n iliyopitia mimi kwenye maisha yangu na kujifunza au kupambana na kutatu ni tofauti na Dada yako au Pengine Wazazi wako ukiwachanganya pamoja(hihihihi this sounds ka' tusi) na hata Mwalimu wako! Najua Mengi Kimaisha lakini sijui Kila kitu.
Hivyo huwa sishangai au kumkejeli yeyote ambae anaushauri/jibu kwenye kila jambo au mambo mengi(wewe huamini kuwa mtu huyu mmoja anaweza kupitia yote hayo maishani). Kuna Magonjwa mtu amekabiliana nayo, ambayo watu wako hawajawahi kuugua. Kuna changamoto nyingi tofauti alizopambana nazo katika maisha yake nakushinda wewe hutokaa uzipate, Huenda anafanya kazi kwenye jamii na hivyo anakutana na Mengi anapokuwa kazini na hivyo kujifunza even more!
Sio hayo niliyoyataja tu bali kuna mengine anashuhudia na kuhusishwa na ndugu/jamaa zake ambao wanapatwa na matatizo ya Dunia, na yeye akajifunza, sasa badala ya kumsimanga/mcheka/kejeli mtu kuwa "anajifanya" anajua kila kitu au kumshangaa "haiwezekani ajue kila kitu" kumbuka na zingatia hili Mwalimu Bora Duniani ni Uzoefu wako Binafsi pia Mengi sio Yote!
Ahsante kwa muda wako hapa, Nathamini na kuheshimu uamuzi wako wa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments