Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kujiswafi

Kijinyama/Ngozi kutoka K-ini...

...pengine hujawahi kuambiwa kuhusu hili la "kijinyama", "Kijingozi" lakini lipo na huwatokea wanawake wengi tu, tatizo ni kuwa wengi hawapendi kulizungumzia.....Uanake ni zaidi ya Makeup, Matiti na Kuvaa Magauni na Blauzi. Umewahi kujiswafi na ukakutana na kitu cha ajabu ukaanza kuogopa n a kudhani Kizazi kimetoka(hahahaha) au Mimba imeharibika bilakujua kama ulikuwa  nayo au ukadhani Umelogwa ili upate Hedhi ya Manyama badala ya Damu? Mara nyingi hii hutokea mara tu baada ya Kumaliza Hedhi na kufanya Mapenzi, au pengine umefanya Mapenzi na Mwenza akaenda "mbali" na baada ya kumaliza ukaona Damu na baada ya kujiswafi ukatoa "kijinyama" ambacho hakiterezi kama Ute Mzito au Damu nzito......usiogope hasa kama Umeruka Hedhi. Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke Ukuta wa Mji wa Uzazi(Uterus/Womb) hujijenga kila baada ya siku 23 na baada ya hapo  hung'oka na kuteremka sambamba na Damu pale unapokuwa Hedhini....sasa ikiwa umepitiliza au

Usafi na Kinyaa....

Ni vitu mbili tofauti....Natumai umeamka/shinda salama. Mtu kuwa msafi haina maana ana kinyaa na mwenye Kinyaa sio kwamba ni msafi pia....japokuwa wapo wasafi na wanakinyaa pia(mie).....hivi ni kinyaa au uoga wa kupata maambukizo? Nakumbuka nilipokuwa nakwenda Hospitali kwa matibabu au kumtembelea Mgonjwa....nilikuwa naumwa kichwa balaa. Nikitoka tu maeneo ya Hospitali napona. Natabia ya kubana Mkojo kwa muda mrefu(usijaribu hii ila kama ni mtu wa Kuendiketa poa) ili nisitumie vyoo vya wote(public)....Haja kubwa (sorry 4 TMI)huwa haiji nikiwa kwa watu au nje ya kwangu/kwetu.....hii sasa ni Saikoloji issue. Jana nimetoa siri yangu kwa Asali wa Moyo kuwa tukienda kwa watu(ndugu zake incl) huwa siogi wala kutumia vifaa vyao vya kujisafishia. Nitafungua Shower vema tu au kujaza Ndoo maji(inategemea nipo wapi) na kuacha shower iendelee au kumwaga maji as if naoga kumbe nanawa miguu...hihihihi. Badala ya kucheka akabaki kaduwaa hehehehehe well sina siri tena maana hata wewe msoma