Skip to main content

Scandals: Binti ajiua kisa B'friend+...Miaka 20 Tangu Secondary!

Hello tena, karibu  tuendelee na "series" sehemu ya maisha yangu ya Shule.


Baada ya Muda si watu wakaanza ku-date bana.....unasikia tu gossip kuwa fulani anatoka na fulani, tulipotoka wao walienda kujibanza kwenye ma-bin na kufanya yao. Unaangalia Darasani(wa Asubuhi na Mchana) huoni hata Kijana wa kutoka nae(hakuna anaekuvutia(well mie nilikuwa mdogo Sec, 1st Bf alikuja nilipomaliza Kidatoo cha Nne huko mbele....Team Wasiona haraka. Achana na hili!

Kanisa la Mtakatifu Joseph




Wanafunzi wa nyuma yangu walikuwa Mapepe sana, na wengi walitokea palepale (Forodhani Msingi) hivyo walikuwa na Mahusiano na Wakaka wa Vidato vya juu  na mmoja wao aliekuwa akipiganisha Wadada wa kila Shule pale Mjini. Aliitwa JJ (sitasema alipokuwa akiishi wala alivyofanana)....alikuwa Mbele yangu Kidato. Huyu jamaa alikuwa napiganisha sana Mabinti wa Msingi na Wale wa Secondari(si unajua kuwa Foronda kuna Msingi na Sekondari eeh). Mwaka wao hawa akina JJ kulikuwa na wakaka "fresh" kweli(Watanashati/Ma-handsome).






Basi siku tumeingia Getini tunasikia watu wanalia, kulikoni? kuna taarifa Binti wa Kidato cha Pili amefariki(amejiua) kwasababu Mpenzi wake kamkataa.....Mpenzi wake ni nani? JJ....aiii Mie kama mie nikamuona yule Binti Bwege kweli, huyo JJ mwenyewe sio m-hot kiviiile(enzi hizo hatukuwa tunatumia neno Hot hihihihi).





Polisi wakaja wakamkusanya JJ "for protection" na hatukumuona tena mpaka baada ya Wiki 2.....huku nyuma bwana kama kawaida watu tukaanza kuchangishwa Senti za Rambirambi na baadae kurudishwa Nyumbani....yeah Ulaya Mwanafuzi mwenzenu akifa mnapewa "Kanselazi" wawasaidie kupokea Msiba Kisaikolijia , sie tukarudishwa tu nyumbani na mimachozi na mawazo na uoga wetu dhidi ya "mtu kujiua".




Kesho yake, Shule ikaendelea kama kawaida halafu siku ya Kuzika ikafika....likaletwa Couch(yale ya Sarafi ndefu yale Mazuriiii, watu walikuwa na mbwembwe)  la kutupeleka Mazikoni tukiwa Ndani ya Sare za Shule kama kawaida(mie sikwenda though).




Msiba wa Binti huyo ulinisumbua sana akili kwasababu nilikuwa sielewi kwanini hasa mtu ajiue kwa sababu ya Mvulana! Mvulana anakupa nini mpaka ukimkosa unaamua kuishi basi eh? Anyway Mungu aendelee kumrehemu yule Binti(sijamtaja kwa sababu ya Kuheshimu Familia yake).




Scandals zilikuwanyingi sana pale Shuleni, Kuna Mwalimu na rafiki ya Baba yangu(Mungu akurehemu Dingi) aah Mwalimu Marehemu "D"mkali wa Hisabati(halafu sijui Hesabu wala nini), maskini alifariki siku chache kabla ya kufunga Ndoa na Mwalimu mwenzie(mkimama wa Kihaya alikuwa muzuriiiii na anamadoido utafikiri hachutami kukamua Kimba) ambe ilisemekana alikuwa na "gundu".....kila anaemchumbia hufa siku chache kabla ya Ndoa.




Scandal nyingine ilikuwa ya Binti Mmoja wa Kizungu(alizushiwa kafa kwa Ngoma)....alikuwa Mwaka wa akina JJ....alikuwa Kiwembe huyo hihihihi....huyu alitoweka ghafla tu.



Kuna Scandal ya Jamaa moja hivi ambalo lilikuwa linachukia Wanawake lakini wanawake walimpenda so alikuwa akiwakubali na akienda nao huko anakowapeleka anawafanyia "dharau" ili wasimsumbue tena.....hihihihihi ningekutajia ila wacha nmstahi tu(atakuwa kazeeka sana sasa maana alikuwa wale repeat-ers).....unapiga Darasa la Saba mara zote mpaka Ufaulu.



Pia kuna yule Binti wa Kizungu alikuwa Kiwembeee, akazushiwa kuwa na HIV,,,,,,akatoweka ghafla. Miaka 3 baadae watu wakasema amefariki.


Kulikuwa na Watoto wa Pembeni(nje) wa wakubwa wa Inji yenu pale shuleni kwetu, kuna Mdada alikuwa Bingwa wa kupata Mitihani kabla haijafanywa hehehehe, kila Mtihani yeye anatuacha Mita 200....halafu alikuwa Mnoko na Msongo(hacheki ovyo-ovyo) balaa huyo Mdada.





Mwaka 2005 (sikumbuki vema) nikakutana nae ndani ya Ndege ya Ethipia....nkamsemesha, akajifanya hanijui hihihihi. Nkamwambia well tulisoma wote....so unafanya nini UK? akasema anasoma....Nkaongeza wee baba yakoWaziri sasa kwanini unapanda Ndege ya walala hoi? akasema ndio flight pekee iliyopatikana haraka.....kumbe mie sikujua Baba'ke alikuwa na Scandal ya Ufisadi sijui nini na nini na yeye alikuwa anarudi kimya-kimya ili kuua "uzushi".....hihihihi. Oh yeye alikuwa Mtoto wa Mkufunzi sio wa pembeni enzi hizo tupo Shule.....nimechomekea hadithi(mambo ya Live Tv haya nayo hehehehe).





Enhee yule Mwalimu wetu yule Mkali wa Physics(nimemsahau, nili-drop PCB nkaenda Biashara), alikuwa fashionable sana pia ufundishaji wake ni wake- naughty-naughty hivi hihihihi alikuwa anatengeneza Pesa nzuri, maana alifundisha Madarasa ya Ziada Mapaka Usiku....huyu nae alikuwa kiWembe mpaka Mkewe (mwalimu pia) akahamia Forodhani kulinda mali zake.





Talking about kuchukua Biashara, kulikuwa na Limjamaa (Mwalimu wa Bookkeeping) abuser kweli....Wanafunzi wa mbele yetu walikuwa wanasema kwamba Jamaa akikutaka na ukamkataa basi atakuwa anakuchapa Daily bila sababu.....by the time nafika Kidato cha Tatu Maombi yangu kwa Mungu baba yalikuwa Mwalimu huyo sijenitaka mimi. Kwa bahati nzuri au mbaya kukawa na Mgomo wa Walimu wa Secondari na yeye akaacha kufundisha akaenda Kutangaza Radio(ile ya Kanisani palepale Forodhani).



Hizi ndio Scandals nilizozikumbuka siku hii ya leo. Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa.ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao