Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!! Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie. Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye! Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaani wanasubiri k