Skip to main content

Posts

Showing posts with the label malkia

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...

...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani? Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme. Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme  kama uliikosa. Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe. -Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa

Mke anafanyiwa mapenzi, sio the other way around!

Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!! Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie. Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi  kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine  nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini  na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye! Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaani wanasubiri k