Monday, 3 July 2017

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...


...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani?


Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme.


Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme kama uliikosa.


Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe.

-Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa urahisi lakini atakuwa "suprised" na andika "hizi zako, tumia utakavyo", kwa Mfano. Badili ujumbe kila mara unapofanya hivyo.


-Onyesha/toa Shukurani kwa  kazi yake ngumu ya kutoa Malezi mazuri anayowapa watoto, hasa pale unapoona Watoto wanajiamini lakini wana Nidhamu(kuna tofauti kati ya kujiamini na kuwa mtovu wa Nidhamu), kama ni Mama wa Nyumbani. Kumbuka Malezi ni jukumu lenu w ote kama Wazazi lakini kwa Kawaida Mama huchangia zaidi ya Baba, hasa kama Mama huyo ni wa nyumbani.

-Onyesha(onesha) unajali anapokaribia na anapokuwa Hedhini, jifunze namna ya kumpa support, kipindi hiki huwa kigumu kwa baadhi ya Wanawake kama ambavyo ma-teenager huwa japokuwa ni kwa muda mfupi.

-Sifia Mapishi yake na sema Ahsante kila anapokuandalia chakula.

-Usishindane au kulinganisha  "attention" anayotoa Mama kwa  Mtoto/Watoto wenu, wewe ni mtu Mzima unaweza kujihudumia. Watoto bado wanajifunza na wanahitaji "attention" zaidi yako. Mkeo sio Mama yako bali  Mpenzi wako ambae pia ni Mama wa Watoto wenu. Usisahau.

-Mpeleke Manunuzi(Madukani) kila baada ya Muda fulani....sio kwenda kununua Chakula bali mahitaji yake binafsi kama vile Vipodozi, Manukato. Pads n.k,

-Anapokuambia  jambo "serious" hata kama sio hivyo kwako. Msikilize mpaka Mwisho ndio uulize swali, usiulize maswali katikati kabla hajamaliza anachokuambia. au Jitahidi kumsimamisha kwanza alafu ndio uulize....usiulize kwa kuingilia. hii itakusaidi kumuelewa zaidi.

-Jifunze Mzunguuko wake wa Ngono ambao unaenda sambamba na wa Hedhi...zile siku ambazo anakaribia ndio muda Mzuri wa wewe "kulianzisha"....kwa muda wa siku 12 tangu Hedhi kuisha Mkeo hupoteza hali ya kutaka Tendo, sio kwamba hatamani bali anahitaji "msaada" ili kutaka Tendo hivyo ongeza ujuzi kwenye kumuandaa ili kumsaidia kufurahia Tendo atakapokuwa tayari.

-Onyesha au sema adharani kuwa yeye ndio Boss....mf; Dukani, mmenda kununua Kapeti au Gari, pamoja na kuwa Muuzaji anasisitiza ununue na unajua umelipenda lakini Mkeo anaonyesha kusita, mwambie Muuzaji "huyu ndio Boss wangu, Uamuzi wake ni wa Mwisho".

au Mmekutana na "Rafiki" yako ambae hamjakutana kwa  muda mrefu, rafiki anakuomba mkutane Pub, wewe hukupanga kwenda huko siku hiyo, unamrushia Mpira Mkeo..."Mpenzi ulisema baada ya hapa unataka kwenda wapi?".....mkeo atasema atakako hata kama hakuwa na mpango huo, atajua kuwa hutaki kwenda Pub na huyo Mtu.

-Muachie afanye maamuzi kwenye mabadiliko ya Nyumba(ndani), Mambo ya kununua Pazia, Sahani, Sufuria na Mashuka haikuhusu.

-Punguza ukaribu au poteza marafiki wote wa Kike, hata kama ni Dada zako(just saying, females are snakes, I don't even trust myself kama Wifi/Rafiki kwa Wanaume hihihihi).

-Msabahi na Muage kwa Busu na/au Kumbato.....usisahau kumpigia  Simu kumjulia hali unapokuwa mbali na Nyumbani.

-Mueleze(wasiliana) kwa uwazi kuhusu Hofu zako, Shida zako....misukosuko ya Kikazi/Biashara. Hakuna mambo ya "kiume nakabiliana nayo mwenyewe"huyo ni Mkeo ni upavu wako, mshiriki wako, Mshauri na mtu pekee anaweza kukusikiliza na pengine kukusaidia kuondokana na baadhi ya "mambo ya Kiume".

-Usimkosoe/Fokea kabla hujaua sababu ya yeye kufanya alichokifanya au kilichopelekea Mtoto kuumia ambapo wewe unadhani ni Kosa, jifunze kuwasiliana bila kumfanya Mkeo ajisikie vibaya.


Nisikuchoshe si eti?

Una swali? shoot at me on dinahicious@gmail.com. Kumbuka nitakujibu  hapa kwa faida ya wengine wenye swali kama lako na sio kwa Email. Shukurani kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa nathamini na kujali Muda wako hapa.


Bai.

No comments: