...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani? Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme. Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme kama uliikosa. Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe. -Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa