Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kufanyamapenzi

Kufananisha/linganisha relationship...

 ,,,au yaliyopita si ndwele tugange ya jayo? Ikiwa umetoka Kimataifa (mbali sio nchi za jirani) halafu baadae ukajaribu nyumbani na kubaki huko kimapenzi ili kuepuka kufuta Race ya watu weusi unakuwa na uzoefu tofauti au tuseme kacha ya kupendwa na kujaaliwa na akupendae tofauti kabisa. Ni kama vile mategemeo yako(maisha uliyozoeshwa) yanakuwa hayana nafasi, sometimes unaeza  jaribu kuyafanya wewe badala ya ku-receive ukitegemea mweza atakusoma ili akupe upatiacho? unatoka bila. Mwanzoni kabisa unaeza usijali sana kwasababu penzi ni upofu obviously, ila jinsi mahusiano yanavyozidi kukua nakuota mizizi unaanza kugundua kuwa watu wa nchi za mbali wanajali zaidi na wanaonyesha mapenzi zaidi kuliko wa nyumbani(inawezekana wanaogopa kuonekana wabahuzi). Kwa kawaida unaambiwa usifananishe/linganishe ila kama ulikotoka huko Mataifa ya mbali kulikuwa ni furaha  na "kula bata" zaidi ya maumivu kihisia na huzuni...unajikita tu unarudi na kuanza kukumbukia(hulinganishi bali unakumbu...

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak...

Kufanya Mapenzi(Ngono) Hakujengi Ndoa yenye Furaha......

....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini? Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na  ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu. Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako  Mkimama basi tena hana Ha...

Mke anafanyiwa mapenzi, sio the other way around!

Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!! Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie. Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi  kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine  nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini  na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye! Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaan...