....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini?
Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu.
Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako Mkimama basi tena hana Hali. True Story!! turudi kwenye Topic...
...Ngono (Kufanya Mapenzi) ni Madhara ya Ndoa yenye furaha.....unajua, kila kitu kina Faida na Madhara yake si ndio? Sasa faida za Ndoa zipo nyingi lakini Ngono(kufanya Mapenzi) sio moja wapo. Kufanya Ngono(Mapenzi) ni Madhara ya kuwa na Ndoa yenye furaha. (Hiki kipengere kimejirudia....Usijali, kuandika na kueleweka sio kazi rahisi kama udhaniavyo)!
Kwamba, ni lazima Madhara hayo yakupate ikiwa Ndoa yako imesimama Imara na imejawa/egemea Upendo, Furaha na yale yote Mema mlioelekezwa, funzwa, jifunza n.k. Pamoja na kusema hivyo bado Ngono(kufanya Mapenzi) haipaswi kufanywa Kila siku. Ikifanyika kila siku inapoteza "Mngaro"? hihihihi mnapoteza "ubunifu" a.k.a mnaishiwa!....
......ndio hiyo inatoka kwangu Mie yule wa Enzi pale Dinahicious, ambae nilikuwa nawashanga sana Watu wanalala vipi Kitanda kimoja bila kupandana kila siku angalau Mara 3. Achana na hili. Mnapokuwa kwenye Ndoa mambo mengi hutokea, kumbuka mmeunganisha Familia mbili tofauti. Kila familia hukutwa na issues zake ambazo huwahusisha ninyi pia kwa pamoja. Kwamba likija kutoka kwenu ni lake na likija kutoka kwa Mumeo pia ni lako. Ukiachilia hayo kuna Malezi ya Watoto na Majukumu Mengine kibao ya Kimaisha.
Sasa mnapoishiwa "Mngaro" au Ubunifu ni wazi kuwa mtakuwa na kazi ya ziada ya kutafuta mambo Mapya ambayo katika hali halisi ni yale yale tu sema hamjayafanya kwa muda Mrefu, but Muda wa kufikiria on how to actually do it tena unagharimu kwani tayari Masaa 24 yapo full....ni kama vile hayatoshi.
Hivyo ni Muhimu kufurahi pamoja bila kukutanisha Miili nakufanya Mapenzi Daily(mara 3-4 kwa Wiki inatosha), kama bado au ulikuwa hujui basi jaribu kujifunza kuwa karibu nae:-
1)-kuonyesha Mapenzi kwa Vitendo popote mlipo bila kuingiliana, Busu, shika/gusa kwa Huba, Mahaba yaani kuwa "Intimate".
2)-Kiroho-kujadili Imani yenu/zenu na Kusali pamoja.
3)- Kiakili-Kufanya Mazungumzo ambayo hayahusiani na Watoto/Kazi/Ndugu.
4)-Ongezea as you go.....
Mpaka umefika hapa ni matumaini yangu kuwa umenielewa au tumeelewana. Kama bado basi usisite kuni-Tweet nami nitafanya Blog Post ingine Spesho kwa ajili yako.
Nathamini Muda wako mahali hapa na Ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments