Skip to main content

Posts

Showing posts with the label furaha

Kufanya Mapenzi(Ngono) Hakujengi Ndoa yenye Furaha......

....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini? Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na  ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu. Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako  Mkimama basi tena hana Ha

Wale akina Wanangu Come First....

Hakika! wao kwanza kabla ya watu wengine baba yao included(hello Asali wa Moyo hihihihi). Hata mie nimewahi kusema/kuwaambia watu kuwa Wanangu kwanza halafu wengine na mengine ndio yanafuta. Nakumbuka nilikuwa na mwambia Mama, "nikija kuwa na mtoto, sitoruhusu mtu amshike....hata baba yake" hapo nilikuwa sijui Uchungu wa Mtoto wala Emotional connection na Bond kati ya Mimba/Mtoto na Mama. Nilihisi kuwa mtoto yupo Salama zaidi akiwa na Mama(nadhani ni Nature tu). Baada ya kuwa Mama hakika Wanangu waka wa kwanza kabla ya lolote kubwa au dogo. Maisha yangu yakazunguukwa na Wanangu na kila kitu kinachowahusu. Ikafikia mahali nikaanza kuhisi sifurahii hii "biashara" sijui "kazi" ya kuwa Mama. Ikawa too much mpaka nikasahau mimi ni nani. Nikasoma mahali (ukinipa mtihani wa Mimba, Kuzaa na kukabiliana na shida/mabadiliko ya kuwa  Mama early days baaya ya kuzaa nafaulu zaidi ya Kufaulu), maana sijawahi kusoma in my life kama nilivyosoma/ninavyoso

Best Umri wa kufurahia Maisha.

Habari yako? Je kuna umri uliopita na ukadhani ulifaidi sana na kufurahia maisha kuliko sasa au miaka michache kati kabla ya umri ulionao sasa? Sijawahi kufanyiwa au kufanya sherehe ya siku ya Kuzaliwa sio tu kwa sababu za Kikacha kuwa hatuna hizi mambo (unaiga tu) lakini pia binafsi sipendi mikusanyiko ya watu na ikiwa naeza kuepuka kwa kutokuwa na Party basi na iwe hivyo....so yeah. Naishi kwenye Nchi ambayo kutimiza miaka fulani ni big deal na hivyo mhusika kutaka ku-share siku yake maalum na watu wengine. Hiyo ni Kacha yao na hivyo inawafanya (Kazini wanajua DoB na anuani yako so huna jinsi)baadhi wanipatie zawadi na hapo ndio suala la "am too old for the party ila zawadi napokea" linakuja  badala ya kuzikataa. Kuna umri ambao nahisi nilifurahia zaidi maisha yangu na hivyo kuzipenda namba au umri huo uliopita. Sikuwa chini ya Wazazi na sikuwa na majukumu. Nilifanya maamuzi bila kujali watu wengine....Baada ya hapo nikawa busy  na maisha. Tangu Kibibi(princess) ameac