Habari yako?
Je kuna umri uliopita na ukadhani ulifaidi sana na kufurahia maisha kuliko sasa au miaka michache kati kabla ya umri ulionao sasa?
Sijawahi kufanyiwa au kufanya sherehe ya siku ya Kuzaliwa sio tu kwa sababu za Kikacha kuwa hatuna hizi mambo (unaiga tu) lakini pia binafsi sipendi mikusanyiko ya watu na ikiwa naeza kuepuka kwa kutokuwa na Party basi na iwe hivyo....so yeah.
Naishi kwenye Nchi ambayo kutimiza miaka fulani ni big deal na hivyo mhusika kutaka ku-share siku yake maalum na watu wengine.
Hiyo ni Kacha yao na hivyo inawafanya (Kazini wanajua DoB na anuani yako so huna jinsi)baadhi wanipatie zawadi na hapo ndio suala la "am too old for the party ila zawadi napokea" linakuja badala ya kuzikataa.
Kuna umri ambao nahisi nilifurahia zaidi maisha yangu na hivyo kuzipenda namba au umri huo uliopita. Sikuwa chini ya Wazazi na sikuwa na majukumu. Nilifanya maamuzi bila kujali watu wengine....Baada ya hapo nikawa busy na maisha.
Tangu Kibibi(princess) ameacha kunyonya full time nimeanza kufurahia Maisha tena, kwamba sasa nalala up to masaa 8! Hakuna kuamka-amka mara kadhaa kila usiku.
Naweza kumuacha na Baba yake jikaenda huko kwa masaa kadhaa bila kuhofia Matiti kujaa au Yeye kuwa na njaa......ni raha tupu!
Nimeisha kuwa wazi kuhusu suala la watu kupata hisia ya guilt kusema ukweli kuwa hawafurahii kuwa Mama(baada ya kuzaa).
Kama unalala masaa 4 ya kukatisha na upo on the go na wanao wawili chini ya miaka 5 na unafurahia Maisha yako basi wewe ni vere vere spesho au sio wa Dunia hii.
Babai.
Comments