Kwa wale ambao Uhusiano wa bf na gf uliharibika na kuvunjika kwa sababu zozote na kwa bahati mbaya mlizaa (ukizaa na mtu halafu ni X mwenzangu ni bahati mbaya).
Sasa imagine kila unapowakorofisha watoto......watoto hukasirika tu hata kwa yale mema kwao.....mf unawakataza wasicheze Jikoni ni hatari au unahimiza wafanye home work badala ya kutazama Tv.
Kila unapokwenda kinyume na watakavyo kama mzazi kwa faida yao wanaanza kulia au kununa na kumtaja mama au baba yao......"Baba angekuwepo ingekuwa hivi au vile" au "mama angekuwepo asingenikataza hili au lile" na hiyo huwaongezea huzuni na hata kilia kwa Uchungu bila wewe kuwaona.
Mara chache unaweza kusikia wakimtaja mzazi mwenzio ambae ni mama au baba yao lakini umeachana nae na sasa unamchukia.
Nimesema hayo yote kutokana na tabia ya Babuu pale unapomuudhi(ukimkataza kufanya kitu).....ananuna halafu anasema "I want my dad to come and cheer me up".
Maneno hayo hunifanya nimuonee huruma (ndio atakacho) na kujisikia vibaya......halafu nawaza....Baba yake angekuwa Ex wangu.....yaani alinikimbia baada ya kushika Mimba aiiii mbona ningemkunyuga (chapa) huyu mtoto aisee. Well ningekasirika tu nisingempiga.
Sasa wewe uliepo kwenye situation hiyo ya u-single baba/mama huwa unakabiliana vipi na hili? Huwa hupati mahasira kweli watoto au mtoto anapoleta the ex factor?
Usi panic mie nawaza tu kwa maandishi.
Babai.
Comments