Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mtoto

Kwaheri Social Media(Twita)...

...hivi YouTube inahesabika kama Sosho Midia?  Kama sio basi Platform pekee naiaga kwa sasa ni Twitter. Sijawahi "kujiunga" na Instagram, Snapchat wala Tiktok. Kwanini? Ukiachilia mbali kuwa Muda unabadilisha watu(wanakua), vilevile vitu na mitazamo hubadilika kulingana na Tabia Uchumi/Nchi/Utamaduni....nadhani Twita imejaa wafanya Biashara kwa kupitia Ajenda binafsi/Harakati, Biashara ndogo ndogo na Biashara Utapeli (ulipie waliojifunza YouTube  bure), Biashara ya Miili(intimate picha/vid) oh bila kusahau Biashara ya "kuomba omba". Baada ya miaka kadhaa, nimegundua kuwa Twita hainifaidishi kwasababu sina Biashara(sikuzi Brand), hivyo sihitaji kuwa active na ku-engage na followers every few hours on daily. Kabla ya hapo nilikuwa Active sana kwenye Masuala ya Kisiasa(Naunga Mkono Upinzani Tz), baada ya Muda nikajitoa, uamuzi uliopelekea  "kurukia" zaidi issues rahisi rahisi ambazo zimejaa chuki/vita ya Wanawake vs Wanaume, hasira, kutokujiamini,

Miaka 30 ndio mwisho wa kutaja Umri wako...

Kwa mwanamke.....habari za Masiku tele? Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Nilipojuja Nchi hii miaka zaidi ya 10 nilikuwa kwenye my early 20s na nilikuwa nasafiri kama mtoto....sio nilifoji la hasha! Wakata Tiketi waligoma kukubali umri wangu na wakasema mie ni binti wa miaka 15yrs. Nilinilikuwa nakaa Kijijini halafu nasoma London) na Kiingilishi changu cha kudandia akuu mkidada wala sikubisha so nikakata Kibali cha Usafiri kama mwanafunzi wa Kimataifa wa Miaka 15 ambacho ni Chee. Enzi hizo (2000s) hakukuwa na mambo ya kufuatiliana kwenye Passport. FAST FOWARD....nikawa na Mume ambae anakunywa Pombe, nikienda nunua Pombe wanagoma kuniuzia eti mpaka niwe na Miaka 25 hihihihi. Nikiwaambia mie ni mama wa watoto 2 na nipo in my 30s wananicheka na kunambia a 23yr old woman can have a child too so wanaomba  niwaonyeshe kithibitisho cha umri(Driving License) nawaonyesha.....misamaha mingi ikijumuishwa na hongera kwa kuluku so yang'i. Au kwa maana nyingine am a 23yr old who look like a

Mwanao anapoleta the Ex Factor

Kwa wale ambao Uhusiano wa bf na gf uliharibika na kuvunjika kwa sababu zozote na kwa bahati mbaya mlizaa (ukizaa na mtu halafu ni X mwenzangu ni bahati mbaya). Sasa imagine kila unapowakorofisha watoto......watoto hukasirika tu hata kwa yale mema kwao.....mf unawakataza wasicheze Jikoni ni hatari au unahimiza wafanye home work badala ya kutazama Tv. Kila unapokwenda kinyume na watakavyo kama mzazi kwa faida yao wanaanza kulia au kununa na kumtaja mama au baba yao......"Baba angekuwepo ingekuwa hivi au vile" au "mama angekuwepo asingenikataza hili au lile" na hiyo huwaongezea huzuni na hata kilia kwa Uchungu bila wewe kuwaona. Mara chache unaweza kusikia wakimtaja mzazi mwenzio ambae ni mama au baba yao lakini umeachana nae na sasa unamchukia. Nimesema hayo yote kutokana na tabia ya Babuu pale unapomuudhi(ukimkataza kufanya kitu).....ananuna halafu anasema "I want my dad to come and cheer me up". Maneno hayo hunifanya nimuonee huruma (ndio atak