...hivi YouTube inahesabika kama Sosho Midia? Kama sio basi Platform pekee naiaga kwa sasa ni Twitter. Sijawahi "kujiunga" na Instagram, Snapchat wala Tiktok.
Kwanini? Ukiachilia mbali kuwa Muda unabadilisha watu(wanakua), vilevile vitu na mitazamo hubadilika kulingana na Tabia Uchumi/Nchi/Utamaduni....nadhani Twita imejaa wafanya Biashara kwa kupitia Ajenda binafsi/Harakati, Biashara ndogo ndogo na Biashara Utapeli (ulipie waliojifunza YouTube bure), Biashara ya Miili(intimate picha/vid) oh bila kusahau Biashara ya "kuomba omba".
Baada ya miaka kadhaa, nimegundua kuwa Twita hainifaidishi kwasababu sina Biashara(sikuzi Brand), hivyo sihitaji kuwa active na ku-engage na followers every few hours on daily.
Kabla ya hapo nilikuwa Active sana kwenye Masuala ya Kisiasa(Naunga Mkono Upinzani Tz), baada ya Muda nikajitoa, uamuzi uliopelekea "kurukia" zaidi issues rahisi rahisi ambazo zimejaa chuki/vita ya Wanawake vs Wanaume, hasira, kutokujiamini, kukata tamaa, kutangaza Maradhi, Uchochezi, kujiamini kupita kiasi(Kiburi), kujiona, kujisikia na kutoleana Siri.
Yote niliweza kujichomeka na wakati mwingine kudharau, ilifikia mahala nikawa napata "followers" wengi sana kwa siku....nikaweka Kufuli na kisha ku-"force unfollow" elfu kadhaa.
Aibu Kuu: Siku moja Kijana wangu akalalamika kuwa "Mom you spend too much time on your phone(Twitter), and when we speak to you...you shout".
Nikaogopa! Sikujua kuwa nilikuwa naweka "focus" yangu yote kwenye Twita na kusahau kuwa nina watoto wanaohitaji Muda wangu, kindness na attention yote.
Nikasema, huenda naelekea kuwa Mlevi wa Twita(na tweet/maisha/mawazo ya watu)... nikaamua kuwa-mute wale wote ambao walikuwa wakileta "Drama" kwenye TL yangu ili nisishawishike kuweka neno/maoni na kuvuta followers kusema chini/juu ya twiti zangu.
Kitendo ambacho kilisaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza Muda wangu Twita, nikaweza kupotea kwa Wiki 2, nikapotea kwa Mwezi 1, baadae nikaondoka kwa Miezi 2na. Sasa, nimeamua niondoke kwa Muda mrefu zaidi....Mpaka utakapo niona tena, ahsante sana kwa kuwa nami tangu 2015-2022.
Kama Social Media haikusaidii kutengeneza Pesa, kukuza Personal Brand kwa lengo la kuanzisha Biashara huko mbele, tafadhali limit Muda wako kwenye platforms hizo.
Muda wako ndio unasababisha wamiliki wa Platforms hizo kutajirika(wanauza Muda wako, Data zako kwa Makampuni ili wapate Matangazo). Muda na Bando lako ni Mali, usigawe ovyo(bure) kutajirisha wengine.
Ewe Follower, ubaki salama eti, mpaka utakaponiona tena. MapendoZ.
Alamsiki.
Comments