Skip to main content

Miaka 30 ndio mwisho wa kutaja Umri wako...

Kwa mwanamke.....habari za Masiku tele? Ahsante kwa kuichagua Blog hii.


Nilipojuja Nchi hii miaka zaidi ya 10 nilikuwa kwenye my early 20s na nilikuwa nasafiri kama mtoto....sio nilifoji la hasha! Wakata Tiketi waligoma kukubali umri wangu na wakasema mie ni binti wa miaka 15yrs.


Nilinilikuwa nakaa Kijijini halafu nasoma London) na Kiingilishi changu cha kudandia akuu mkidada wala sikubisha so nikakata Kibali cha Usafiri kama mwanafunzi wa Kimataifa wa Miaka 15 ambacho ni Chee.



Enzi hizo (2000s) hakukuwa na mambo ya kufuatiliana kwenye Passport.



FAST FOWARD....nikawa na Mume ambae anakunywa Pombe, nikienda nunua Pombe wanagoma kuniuzia eti mpaka niwe na Miaka 25 hihihihi.



Nikiwaambia mie ni mama wa watoto 2 na nipo in my 30s wananicheka na kunambia a 23yr old woman can have a child too so wanaomba  niwaonyeshe kithibitisho cha umri(Driving License) nawaonyesha.....misamaha mingi ikijumuishwa na hongera kwa kuluku so yang'i.



Au kwa maana nyingine am a 23yr old who look like a 30something woman....hiihihihi got it? Wadada wa 20s wa sass wanaonekana watu wazima.



Mama yangu alimzaa mdogo wangu wa mwisho akiwa na miaka 35.....hakika nakumbuka mama alivyokuwa so yeah. Hapana that isnt my age! Nakaribia 40 ndio my age(nimevuka 35).


Kuna kijisheria kisicho rasmi cha wanawake kutotaja miaka yao baada ya 25.....hawa huwa na hatari ya kuishi wakiamini bado wanaonekana in their 20s na pengine kushindana na 20s girls hass kwenye ulimwengu wa Sosho midia.


Mie nimeacha kutaja umri wangu baada ya miaka 30. Yaani ukigonga miaka 31 vitu vilivyokua muhimu in 20s havileti maana tena(i wonder why a 40yr  old anadai kuwa anahisi kama a 27yr).



I hope I wont go back to my 20s when i hit 40......nataka kubaki hapa hapa kwenye 30s kihisia na kadhalika.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao