Not exactly.....
MAY Moja njema sana kwako mpendwa na ahsante kwa Kuichagua Blog hii.
Kuna siku nilikuwa nasoma Forum moja hivi kuhusu Ughali wa Maisha hasa kwa sisi Mama wa nyumbani wa Muda mfupi au wale wa Kudumu(sijaji mie).
Mdada mmoja akauliza ni namna gani wenzake wanabajeti vipato vya Waume zao. Yeye akadai kuwa anashindwa kabisa kubajeti Mia Tano Hamsini (£550)kwa Wiki.
Akaja Mmarekani bwana (tatizo la mUS ni la wote si walijua hilo)akaanza kushusha manamba kuwa mumewe anaingiza $750 kwa Wiki na haitoshi ndio itakuwa £550.....siku pay attention kwenye Dola & Pound mpaka nimesoma hii article.
The Guardian: Congress to propose bill raising US minimum wage to $12 by 2020. http://google.com/newsstand/s/CBIw1Iu9zSE
Obviously hata yeye wa $750 hakuiona £ kabla ya 550 hihihihihihi oh boy kumbe Dola 750 is less than Pound 550.....Kima cha chini UK ni £6.45p Labour wakishinda inakwenda 8...kwa maana nyingine US watafikia 6.45p in 5 years......sio exactly lakini you get an idea.
Bado sielewi kwanini Bidhaa za US zikija huku zinakuwa Ghali. Haa! Mie na Hisabati wapi na wapi.
Babai.
Comments