Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mzazimmoja

Single Mum/Loner Parent, Mzazi Mmoja=no Help

Hi! Sitojifanya mjuaji kwenye hili, tangu sijawahi kuwa "single mother" iwe kwa kutaka (wale wanaoamua kushika Mimba bila kuwa na hitaji la mwanaume husika) au kwa bahati mbaya, kwamba kutofautiana kwenu kumefanya mmoja wenu abaki na mtoto/Watoto(hapa siwazungumzii Wajane au wale waliobakwa, hii ni issue nyingine). Ninaowagusia hapa ni wale ambao kuwa "single mother" ni Mtindo wa Maisha,Sifa, chanzo cha kuonekana Imara/Unaweza! Wengi hapa ni wale Wasichana waliokulia miaka ya 90s na wale wa early 2000s. Ule msukumo wa kutaka kujitegemea ukikuwa na "impact" kubwa kwetu kiasi cha kuhisi hatuhitaji Wanaume ili kuwa na Familia. Tuliamini kuwa tunaweza kufanya yetu kama Wanawake na tunaweza kufanya ya Wanaume pia, "ikiwa mwanaume anaweza hata mimi naweza" sort of Imani....hakika hakuna afanyacho Mwanaume ambachoo sisi hatuwezi kufanya, lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya kama Wanawake kwenye malezi ya Mtoto au watoto(h

Mwanao anapoleta the Ex Factor

Kwa wale ambao Uhusiano wa bf na gf uliharibika na kuvunjika kwa sababu zozote na kwa bahati mbaya mlizaa (ukizaa na mtu halafu ni X mwenzangu ni bahati mbaya). Sasa imagine kila unapowakorofisha watoto......watoto hukasirika tu hata kwa yale mema kwao.....mf unawakataza wasicheze Jikoni ni hatari au unahimiza wafanye home work badala ya kutazama Tv. Kila unapokwenda kinyume na watakavyo kama mzazi kwa faida yao wanaanza kulia au kununa na kumtaja mama au baba yao......"Baba angekuwepo ingekuwa hivi au vile" au "mama angekuwepo asingenikataza hili au lile" na hiyo huwaongezea huzuni na hata kilia kwa Uchungu bila wewe kuwaona. Mara chache unaweza kusikia wakimtaja mzazi mwenzio ambae ni mama au baba yao lakini umeachana nae na sasa unamchukia. Nimesema hayo yote kutokana na tabia ya Babuu pale unapomuudhi(ukimkataza kufanya kitu).....ananuna halafu anasema "I want my dad to come and cheer me up". Maneno hayo hunifanya nimuonee huruma (ndio atak