Hi!
Sitojifanya mjuaji kwenye hili, tangu sijawahi kuwa "single mother" iwe kwa kutaka (wale wanaoamua kushika Mimba bila kuwa na hitaji la mwanaume husika) au kwa bahati mbaya, kwamba kutofautiana kwenu kumefanya mmoja wenu abaki na mtoto/Watoto(hapa siwazungumzii Wajane au wale waliobakwa, hii ni issue nyingine).
Ninaowagusia hapa ni wale ambao kuwa "single mother" ni Mtindo wa Maisha,Sifa, chanzo cha kuonekana Imara/Unaweza! Wengi hapa ni wale Wasichana waliokulia miaka ya 90s na wale wa early 2000s. Ule msukumo wa kutaka kujitegemea ukikuwa na "impact" kubwa kwetu kiasi cha kuhisi hatuhitaji Wanaume ili kuwa na Familia.
Tuliamini kuwa tunaweza kufanya yetu kama Wanawake na tunaweza kufanya ya Wanaume pia, "ikiwa mwanaume anaweza hata mimi naweza" sort of Imani....hakika hakuna afanyacho Mwanaume ambachoo sisi hatuwezi kufanya, lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya kama Wanawake kwenye malezi ya Mtoto au watoto(hasa wa Kiume).
Nakumbuka mimi mwenyewe niliwahi kusema kwenye Moja ya Forums kuwa, sitaki Mume na ikifikia mahali nahisi kutaka Familia basi "nitabaka" Mwanaume aka kujilengesha ili nishike Mimba, na nikifanikiwa basi sitomwambia huyo jamaa na hivyo kunirahisishia mimi kumlea "mwanangu" bila Baba yake. Nilikuwa young and stupid early 20s girl, sikufikiria hisia za Mtoto na kiukweli sikuwa nawaza kuwa siku moja nitakuwa mama so ilikuwa "chat" tu....lakini kwa wakati ule nilimaanisha.
Ni vema tutambue kuwa, Mungu ametubariki(sileti ulokole hapa usikimbie hihihihi) kwa namna tofauti, Mwanamke kabarikiwa kivingine na Mwanaume kabarikiwa kivingine (hatufanani) lakini sote tupo sawa in a different way na tunahitajika sawa sawa kwenye Maisha ya Mtoto/Watoto. Usawa huo hauna maana mmoja wetu anaweza kuufanya kwa kuchukua nafasi ya mwenzie.
Mfumuko huo wa "loner parents", wengi wakiwa Wanawake....umeondoa thamani ya Maisha ya Familia, kwamba watu hawajali kuwa Familia na badala yake wanajali zaidi kuonekana kuwa wao ni "single parents" na wanataka kutambulika na kusifiwa kuwa ni "Imara na Jasiri" kwa kuchukua Jukumu la Baba wa mtoto. Fuatilia "Fathers Day" uone wamama wanavyoingilia hii siku kwa kutaka "kutambuliwa" kwa kuchukua/fanya majukumu ya Baba. Huwa najiuliza, Majukumu ya Baba ni yapi hasa?
Jukumu la Baba ni yeye kuwepo kwenye Maisha ya mtoto/Watoto, kutumia muda wake na wanae/mwanae, kumfunza kama Baba(kumbuka Mungu ametupa Baraka tofauti kijinsia, hatufanani kiakili so mafunzo yetu kwa watoto ni tofauti pia). Sasa kama Baba hayupo kwenye Maisha ya Mtoto kwasababu zozote zile, bado hufanyi Jukumu la Baba wa Mtoto/watoto husika.
Natambua kuwa Mzazi ni kazi ngumu, haijalishi kama wewe ni "Single Parent" au "Couple Parents". sasa ni wapi hasa unapaswa kujiita "single Parent"? well Kama unafanya kila kitu mwenyewe bila Pesa za Matunzo ya Mtoto kutoka kwa baba yake, Msaada kwa ndugu, jamaa, marafiki, Walimu n.k. kwenye kumfunza na kumuangalia mwanao wakati upo kazini....basi wewe ni SINGLE/LONER Parent(Mother/Father).
Vinginevyo, wewe ni Mama wa Mtoto/Watoto ulionao.....Kuwa single sio Ushujaa, kuwa Single sio sifa. Hakikisha unapata msaada kutoka kwa watu wengine unaowaamini, hata kama kati ya watu hao Baba mtoto/watoto hausiki. Inasikitisha sana kwa Watoto wetu kukua wakiona Mama anafanya kila kitu, hii inawaharibu na huenda ikawapa shida huko mbele kwenye maisha yao ya Kisosho na pengine wakati wa ku-date nakadhalika.
Natambua kuwa kuna Vijana wengi sana ambao walilelewa na Mama tu, lakini kwa wakati ule bado kulikuwa na "father figure"....Wajomba, Baba wadogo/wakubwa(waume wa...) , Babu na hata pengine Kaka kutoka kwa Mama wakubwa n.k. Ila, kutokana na maisha ya leo(sio kwa Ughaibuni tu) wengi tunaishi mbali na watu hao(niliotaja hapo juu) kwa sababu ya kazi au Masomo, hivyo watoto (hasa wa jinsia tofauti na Mzazi anaewalea) hukosa kujua upande wa Pili wa Mzazi wake au hata "wasaidizi" ambao ni watu wa karibu (sio wale unaoajiri).
Kuwa Mzazi sio ushujaa, ni Jukumu lako kwasababu ni wewe ndio uliamua kuleta Maisha ya watu wengien Duniani, sasa kama umeamua kwenda mwenyewe au imetokea kwa bahati mbaya mwenzio kakimbia majukumu yake, hupaswi kujiona Shujaa au kudai Sifa za upande wa pili(wa mzazi) kwa sababu unadhani kufanya majukumu yako kwa mwanao/wanao ni kufanya yako na ya baba yake. Kila mtu ana nafasi yake kwenye maisha ya Mtoto/watoto.
Kuna ule Usemi wangu maarufu (in my head) kuwa una Mume lakini bado ni Single mother.....kwamba unafanya kila kitu na Mumeo amekaa tu au anakuwa "mwanao", unamfanyia kila kitu mpaka kumfunza manners!....Kujitegemea kunapitiliza unaishia kuwa "single parent" japo una Mume/Baba wa watoto wao. Sijui umenielewa.....(mwenyewe sielewi)!
Nili-protect maandishi yangu, mesahau neno la siri ili ku-unprotect na sikuwa na muda wa kuandika upya, so yeah....Sorry! Nashukuru na kuthamini muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua blog hii.
Babai.
Comments