Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kujitegemea

Single Mum/Loner Parent, Mzazi Mmoja=no Help

Hi! Sitojifanya mjuaji kwenye hili, tangu sijawahi kuwa "single mother" iwe kwa kutaka (wale wanaoamua kushika Mimba bila kuwa na hitaji la mwanaume husika) au kwa bahati mbaya, kwamba kutofautiana kwenu kumefanya mmoja wenu abaki na mtoto/Watoto(hapa siwazungumzii Wajane au wale waliobakwa, hii ni issue nyingine). Ninaowagusia hapa ni wale ambao kuwa "single mother" ni Mtindo wa Maisha,Sifa, chanzo cha kuonekana Imara/Unaweza! Wengi hapa ni wale Wasichana waliokulia miaka ya 90s na wale wa early 2000s. Ule msukumo wa kutaka kujitegemea ukikuwa na "impact" kubwa kwetu kiasi cha kuhisi hatuhitaji Wanaume ili kuwa na Familia. Tuliamini kuwa tunaweza kufanya yetu kama Wanawake na tunaweza kufanya ya Wanaume pia, "ikiwa mwanaume anaweza hata mimi naweza" sort of Imani....hakika hakuna afanyacho Mwanaume ambachoo sisi hatuwezi kufanya, lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya kama Wanawake kwenye malezi ya Mtoto au watoto(h

Pale unapokuwa Mke mwema....

....halafu unaonekana sio mwanamke "kamili", kwanini? kwasababu hulalamini-lalamiki pale mumeo anapoacha bafu chafu baada ya kuoga au pengine anachelewa kuamka na kuacha kitanda kipo shagala bagala....(hizi sio kazi za mwanamke ni usafi), huombi-ombi pesa ya manunuzi, Vipodozi wala Salon. Inawezekana upo hivyo kutokana na Malezi/mafunzo uliyopitia au huenda umejifunza kupitia Blogs, maana Siku hizi kuna kila aina ya maelezo yanayotuelekeza namna ya kuwa  Wake(na waume) wema, mengine ni mazuri na mengine yanapotosha.....Akili kumkichwa unapoamua kuchukua na  kujaribu ulichokisoma! Ulalamishi na kutaka jambo/kitu kifanyike pale tunapotaka  ndio  inatufanya wanawake kuwa wanawake (ni sehemu ya uanamke), sasa hayo yakikosekana inakuwa kama vile Mumeo ameoa  mwanaume mwenzie ahahahaha. I mean sawa kujitegemea kiuchumi na kuepuka ulalamishi.....lakini pia tukumbuke kuwa baadhi ya Wanaume hupenda Changamoto Ndoani (sio za kugombana na muumizana mioyo/hisia)! Nat