,,,au yaliyopita si ndwele tugange ya jayo?
Ikiwa umetoka Kimataifa (mbali sio nchi za jirani) halafu baadae ukajaribu nyumbani na kubaki huko kimapenzi ili kuepuka kufuta Race ya watu weusi unakuwa na uzoefu tofauti au tuseme kacha ya kupendwa na kujaaliwa na akupendae tofauti kabisa. Ni kama vile mategemeo yako(maisha uliyozoeshwa) yanakuwa hayana nafasi, sometimes unaeza jaribu kuyafanya wewe badala ya ku-receive ukitegemea mweza atakusoma ili akupe upatiacho? unatoka bila.
Mwanzoni kabisa unaeza usijali sana kwasababu penzi ni upofu obviously, ila jinsi mahusiano yanavyozidi kukua nakuota mizizi unaanza kugundua kuwa watu wa nchi za mbali wanajali zaidi na wanaonyesha mapenzi zaidi kuliko wa nyumbani(inawezekana wanaogopa kuonekana wabahuzi). Kwa kawaida unaambiwa usifananishe/linganishe ila kama ulikotoka huko Mataifa ya mbali kulikuwa ni furaha na "kula bata" zaidi ya maumivu kihisia na huzuni...unajikita tu unarudi na kuanza kukumbukia(hulinganishi bali unakumbukia) kuwa Love doesn't hurt, Uhusiano shouldn't hurt...kuna changamoto sawa ila upande wa pili una-work with you as a team.
Mfano wamataifa ya mbali huwa na tabia ya kuonyesha kujali kwa kukujulia hali, kuuliza hofu zako za kimaisha, kikazi/career na how they can assist? Hii inafanyika mara kwa mara na hivyo inakuwa rahisi kwake kutatua issue yoyote kabla haijakomaa. Kila mwezi unakuta fungu la pesa kwenye Account yako ya Bank, na una kipato chako.
Wa nyumbani mwendo ni amri, ulalamishi, hakuna salamu mpaka ukumbushie, ukikumbusha unaambiwa "si tumelala nakuamka pamoja jamani"....akuulize kuhusu hofu zako utambee, kama hutomvuta umwelezee na kama una bahati unasikilizwa na kupewa ushauri...vinginevyo unapata "whatever you decide its your life"....and you thought you were team hehehe. Ukihitaji pesa kwasababu mwezi huu mahitaji yalizi kipato chako, inabidi umuombe...kabla hujapewa lazima upokee Risala, na ujue kuwa siku moja utakumbushwa ni "jinsi gani anakupaga pesa" Hyuu!
Wakimataifa anaonyesha mapenzi kwa vitendo na kwa maneno, atakushika, atakutania kwa heshima(sio kukudhihaki), atakushtua kwa kukupatia kitu anajua unakipenda, anafuatilia "cues" zako na kujitahidi kurekebisha, mawasiliano na uwazi yanachukua seat ya mbele na atakuaga na atakuambia muda anaotarajia kurudi hata kama unaujua na haujawahi kubadilika n.k. Kama kuna, safari, cheo au mabadiliko/mipango yeyote ile utajulishwa kwanza na kuhusishwa moja kwa moja.
Wanyumbani, anakupenda vitendo wakati wa kufanya mapenzi tu, au mkiwa peke yenu....akikutania basi utakuwa ule utani wa nguoni halafu ni yeye tu ndio anacheka mf; ona tumbo lako lilivyokubwa kama Mtungi wa Lita 25, nakupenda na unene wako kama sanamu la Michelini....(Ulaya hii ni abuse). Kwanini akuage na kukuambia atarudi muda gani wakati ujau? Mabadiliko kazini na plans nyingine huambiwi kwani hayo ni mambo ya kiume.
Unajiuliza "sasa vipi kuhusu kunung'unuana?" I got you....Wakimataifa wepesi na wana spidi ya kutosha ila wamenyimwa stamina, rhythim na umotomoto, ukute wapo vizuri nyanja nyingine ili kufidia? Wanyumbani wanavyo vyote, pengine hii ndio inafanya wa-relax kwenye sekta nyingine.
Kama uzoefu wakomkabla ulikuwa mbaya huwezi kufananishia(I mean kukumbukia) ulikotoka iwe kimataifa au nyumbani kama mambo yalikuwa ya hovyo na hapo ulipo ni zaidi au auheni na ulikotoka. Wanasema uzoefu mbaya hudumu zaidi kuliko uzoefu mzuri....nah, kwenye mapenzi bana ukibahatika unaeza sahau kama uliwahi kuwa na mpenzi kabla, unakuwa born again, all new, satisfied and happy.
Ni rahisi kuwaambia watu "hutakiwi kulinganisha/fananaisha" mahusiano ya watu wengine na mahusiano yako sababu hujui how they are going through ndani ya kuta zao Nne, which nakubali kwa asilimia zote. Ila umewahi kujiuliza kwanini huwa huambiwi "usilinganishe mahusiano yako yaliyopita na uliyonayo sasa" sababu watu wanatofautiana...which nayo nakikubali ila sasa Experience si ni best teacher ama? Unaachaje kulinganisha ulipotoka na ulipo sasa ili ku-evaluate wapi unakosa na jinsi ya kuomba ili u-receive....no? haya basi!
Uliyojifunza mwanzo kwa vitendo (kutoa na kupokea) unayatumia ulipo japo sio guarantee kufanikiwa, kuna wakati inabidi ujitoe mhanga ubadilike na kukubali hali ili kuendana na ulipo sasa. Ni kama vile wewe Mama mwenye watoto kadhaa huwa hulinganishi/fananishi tofauti za kila mimba na adha zake au jinsinulivyo-enjoy na baadae uzazi na hatua za ukuaji wa kila mtoto? I do, mpaka mimba zilivyoingiaga nalinganisha(ga).
Hebu nisikuchoshe, ila nikukumbushe tu kulinganisha/fananisha ni asili ya mwanadamu na Historia haifutwi ila usiyabalaze kwa mwenza wako, baki nayo akilini.
Bai.
Comments