Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kila kitu mie

Enzi tulitongozwa uchochoroni...

Miaka 10 iliyopita mlitongozana kwa texts au kwa sauti baada ya kuona picha, nasikia siku hizi wala hamtongozwi kabisa au nyie ndio mmekuwa watongozaji. Wanawake wamekua wawindaji, watafutaji, wapiganaji....wanaume wanafanya nini?  Basi sie "Mid Gen X" a.k.a Xennials a.k.a MillenX (tulizaliwa 1975-85) tulikuwa tunakimbiliwa huku tunaitwa " oyaa mrembo" au "oyaa dada'ke (weka jina la kaka yako)" au hey Binti (weka jina la Baba yako), kama jamaa humtaki/hakuvutii unakimbia kama athletes au unaingia kwenye nyumba yeyote unatulia mpaka jamaa apitilize au ageuze na kurudi kijiweni, then unaendelea na safari zako au inatokea mtu kwenye nyumba hiyo anakisindikiza so unakuwa pretected. Kama jamaa unamkubali basi unapunguza mwendo so anakufikia haraka.  Mnatembea huku anakuuliza maswali kisha mnafika kichochoroni(hakuna watu wengi) then anashusha mistari yake...unadengua-dengua pale na kujiringisha(hiba ya kike) huku unachora chini au unatafuna kucha...unamuang

Kufananisha/linganisha relationship...

 ,,,au yaliyopita si ndwele tugange ya jayo? Ikiwa umetoka Kimataifa (mbali sio nchi za jirani) halafu baadae ukajaribu nyumbani na kubaki huko kimapenzi ili kuepuka kufuta Race ya watu weusi unakuwa na uzoefu tofauti au tuseme kacha ya kupendwa na kujaaliwa na akupendae tofauti kabisa. Ni kama vile mategemeo yako(maisha uliyozoeshwa) yanakuwa hayana nafasi, sometimes unaeza  jaribu kuyafanya wewe badala ya ku-receive ukitegemea mweza atakusoma ili akupe upatiacho? unatoka bila. Mwanzoni kabisa unaeza usijali sana kwasababu penzi ni upofu obviously, ila jinsi mahusiano yanavyozidi kukua nakuota mizizi unaanza kugundua kuwa watu wa nchi za mbali wanajali zaidi na wanaonyesha mapenzi zaidi kuliko wa nyumbani(inawezekana wanaogopa kuonekana wabahuzi). Kwa kawaida unaambiwa usifananishe/linganishe ila kama ulikotoka huko Mataifa ya mbali kulikuwa ni furaha  na "kula bata" zaidi ya maumivu kihisia na huzuni...unajikita tu unarudi na kuanza kukumbukia(hulinganishi bali unakumbukia)