Skip to main content

Posts

Showing posts with the label uhusiano

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak

Pale Mwenza wako anapobadilishwa tabia na "Rafiki"...

...Mara nyingi watu husema au kuamini kuwa Mtu anapopata Pesa au Kazi mpya inayolipa Vizuri kuliko kazi yake ya Awali huwa anabadilika(nadhani niliwahi kuzungumzia kwanini watu huwa hivyo mwaka jana/juzi). Habari? natumai Uumzima wa Afya. Nirahisi kutodhani kuwa Mtu Mzima hawezi kuwa "influenced" na Mtu au Watu wapya wanaomzunguuka....kwasababu amepita Umri wa miaka 30...lakini kihalisia bado wapo Watu Wazima ambao wamekua Miili tu na Namba zimeongezeka lakini Akili zao bado ni za Kitoto. Bado wanapata hitaji la  kutaka kufanana, ku-fit in, kuwa kama yule/huyu,kukubalika n.k. Inasemekana hali hiyo  hutokana na Ukosefu fulani wa "attention" kutoka kwa Walezi/Wazazi kipindi ambacho Mhusika alikuwa chini ya Miaka 10. Kumbuka matokeo ya Malezi  tuliyopata kutoka kwa Wazazi/Walezi wetu  huwa yanaathiri maamuzi (mabaya/mazuri) na Maisha yetu ukubwani. Mtu anahitaji kitu kidogo tu ku-triger alichokosa Utotoni. Achana na hili. Sasa kwa baadhi mabadiliko huwa Waz

Faida za Kumnunia Mwenza wako....

...Habariyo? Wanawake tunajulikana kuwa tunapenda  sana kununa-nuna si eti? Lakini hata Wanaume pia hununa, ila wao huwa hawaiti "kununa" bali "nataka kuwa peke yangu ili nifikirie" au pengine anaweza kukuambia hajisikiii vizuri au anamawazo. Sote tumetofautiana, jambo dogo kwako linaweza kuwa kubwa sana kwangu, hali kadhalika kauli yako ambayo wewe unadhani ni ya kawaida inaweza kuwa Tusi kuu kwa mwenzio na hata kuhatarisha Ndoa/Uhusiano wenu. Inategemea na Malezi/Makuzi, Mazingira, Uzoefu n.k. Wakati mwingine Kununa is all you need! Biga Mnuno kwa Siku 5(ukizidisha Mkeo/Mumeo ataku-cheat hihihihihi siku ya 6 kidate na ya Saba one night stand....Hisabati Muhimu).....the rule(Bibi yangu alisema), nuna  Maximum Siku Tano tu ukizidisha huna Mume/Mke! Kununa huko hupunguza ukaribu kati yenu kama Mke na Mume, unapokea majibu kwa mkato, ukiingia tu ndani, mmoja anahisi usingizi  ghafla hihihihihi....pia hukupa hisia ya "nampenda" lakini sipendezwi

Je ni lazima atiki viboksi vyako vyote vya Mr wright?

Mwaka ukianza ila mtu hujitahidi kujiwekea List ya mambo/vitu ambavyo angependa kuvifanya au kufanikisha Mwaka husika. Mimi Binafsi kinachobadilika huwa  ni Namba tu na hivyo Mipango yangu huwa haitegemei Mwanzo wa Mwaka. Naweza kuanza Machi nikafanikisha June au nisifanye lolote la ziada kwa mwaka mzima. Furahia maisha huku ukipiga hatua taratibu bila kujiwekea "dead line"(ndio naamini). Pamoja na kusema hivyo bado siwezi kukataa kuwa sote huwa tuna "aina" ya mtu ambae tungependa kubarikiwa enough na hivyo kuwa  nae na kuchangia yale Mazuri, Mabaya na ya Ovyo maishani na hata kuanzisha Familia pamoja. Tena ukiwa katika umri mdogo (miaka 21-30)hali huwa mbaya ziadi.....unatolea  nje watu kibao kwasababu sio "type" yako. Yaani kwnye viboksi 10 anatick 2 tu! Sikuzaliwa tu nikawa 30+ nilipitia unayopitia wewe, na hakika list yangu ya Mr right ilikuwa ndefu kuliko yako.....na hiyo ndio sababu sina List ya Exes kwasababu nilitaka yeyote atakae "

Mke anafanyiwa mapenzi, sio the other way around!

Umewahi kusikia au kusoma mahali Wanaume wakisimulia namna wanavyowafanyia Wake zao na kuapia kuwa Mwanamke nahaitaji kufanyiwa mapenzi zaidi kuliko wao Wanaume, halafu uka-wish kimoyo-moyo Mumeo aje mahali hapo asome na ajifunze?!! Kama ilivyokuwa Dinahicious Blog, kwamba kuna baadhi ya Wanaume walikuwa wakitaka Wake zao wasome Baadhi ya Makala zangu ili wajifunze. Nakumbuka wapo walioniandikia wakisema huwa wanaacha Blog wazi kwenye Simu/Laptops kwa Makusudi tu ili Mke/Mpenzi apitie. Ni muhimu kumfanya Mumeo/Mpenzi wako ajihisi  kuwa ni Mfalme hapo nyumbani kwenu na unaweza kufanya ajisikie hivyo kwa namna nyingine  nyingi na sio kwenye Kufanya mapenzi kila anapokuhitaji/mnapohitajiana/unapomhitaji(siku hazifanani si unajua Homono nini  na nini).....Mwanamke huwezi kufanya yote, mengine mwachie na yeye! Imekuwa ni kawaida kwetu sisi wakimama kutafuta Mbinu za kumfurahisha Mwanaume Kingono zaidi kuliko wao.....wao wakibaba ni kama vile wametulia tu yaani wanasubiri k

Wanawake hatupendani....usimbee awe Jaji sasa!

Sina hakika kama hii ni Imani tu au ni kweli, Naturally Wanawake hawanipendi mie binafsi(imagine ningekuwa mzuri sasa!) ila Wanaume wanananipenda(napatana zaidi na Wakibaba kuliko Wakimama). Kuna siku Mfanyakazi mwenzangu akanijia kwenye Dawati langu akanambia "dinah unajua nakuchukia".....mie nkacheka halafu nikamwambia "sio peke yako, nimezoea kuchukiwa na wanawake"....wewe ungesema is because i am Black! Sasa, hii "wanawake hawapendani" ipo kila Nchi Duniani.....kila mtu anaibuka na sababu yake kwanini hasa hatupendani. Baadhi wanadai ni Wivu wa kike(umbile/kupendeza/mafanikio/kuwa na easylife) na wengine wanasema ni mambo ya Homono tu. Mie sio kwamba nachukia wanawake bali sipendenzwi na tabia ya baadhi ya wanawake wanaofanya maamuzi ya Kipumbavu, kama vile kutojikinga dhidi ya Mimba, au kujitegeshea kushika Mimba ili tu waolewe au wapate sehemu ya Kipato ya Mwanaume husika. Sipendi mwanamke ajishushe ili kuonewa kirahisi. Vilevile