Mwaka ukianza ila mtu hujitahidi kujiwekea List ya mambo/vitu ambavyo angependa kuvifanya au kufanikisha Mwaka husika. Mimi Binafsi kinachobadilika huwa ni Namba tu na hivyo Mipango yangu huwa haitegemei Mwanzo wa Mwaka. Naweza kuanza Machi nikafanikisha June au nisifanye lolote la ziada kwa mwaka mzima. Furahia maisha huku ukipiga hatua taratibu bila kujiwekea "dead line"(ndio naamini).
Pamoja na kusema hivyo bado siwezi kukataa kuwa sote huwa tuna "aina" ya mtu ambae tungependa kubarikiwa enough na hivyo kuwa nae na kuchangia yale Mazuri, Mabaya na ya Ovyo maishani na hata kuanzisha Familia pamoja. Tena ukiwa katika umri mdogo (miaka 21-30)hali huwa mbaya ziadi.....unatolea nje watu kibao kwasababu sio "type" yako. Yaani kwnye viboksi 10 anatick 2 tu!
Sikuzaliwa tu nikawa 30+ nilipitia unayopitia wewe, na hakika list yangu ya Mr right ilikuwa ndefu kuliko yako.....na hiyo ndio sababu sina List ya Exes kwasababu nilitaka yeyote atakae "nigusa bega" lazma atick angalau viboksi 15(who is that pafekiti?).
Jinsi miaka ilivyozidi kwenda ndivyo ambavyo nilikuwa na kua sio, na hivyo kuelewa kuwa unless najiumbia mwenyewe Mwanaume ninae mtaka, hakuna Mwanadamu atatick viboksi vyote 30 vya nimtakae. Kwenye hiyo list hakukuwa na "lazma awe na kazi au pesa" though(I've got my own....well I used to). Pia nilitaka asietaka Watoto(yep sikutaka kuzaa mie kabsaaa).
Nivema kujiwekea Viwango na Ubora wa mtu umtakae na ujitahidi kuwa na list ndefu ya kutosha ili angalau atick viboksi 5.....list yako itakusaidia kuendelea kusubiri zaidi na hivyo kupata muda wa kujijua/tambua na kufurahia Maisha yako kama Binti (kwa wanaume sigusi sababu sijui) kabla hujawa Mke wa, Mpenzi wa na baadae Mama wa.
Nikiwa wazi kutoka rohoni, napenda kukuambia kuwa Penzi la kweli hujitokeza mahali popote, Penzi la kweli halijali "list"....ukimdondokea mtu na yeye akakudondokea hakika "list" yako ya "mr wright" haitoleta maana kwako.
Kwa ninyi young Women (and Men am not judging)ambao mnadhani mnayajua sana Mapenzi na mnajua mtakacho out of Uhusiano kwa sababu ya kusoma love quotes kwenye Social media na kuangalia Tv programs, napengine kuvaba few times.....na sasa mmejiwekea List kwa kuamini kuwa kuna Mr Wright mahali atatick viboksi vyako vyote 20? anza kudhani upya. Kuwa na msimamo na simamia unachoamini lakini usijiwekee limit.....akigonga 5 muhimu kwako kati ya 10, you are good to go....mengine mtajifunnza mbeleni mkiwa pamoja. Fuata Moyo....usiache akili Nyuma.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii, Naheshimu na kuthamini Muda wako Mahali hapa.
Babai.
Comments