Sina hakika kama hii ni Imani tu au ni kweli, Naturally Wanawake hawanipendi mie binafsi(imagine ningekuwa mzuri sasa!) ila Wanaume wanananipenda(napatana zaidi na Wakibaba kuliko Wakimama). Kuna siku Mfanyakazi mwenzangu akanijia kwenye Dawati langu akanambia "dinah unajua nakuchukia".....mie nkacheka halafu nikamwambia "sio peke yako, nimezoea kuchukiwa na wanawake"....wewe ungesema is because i am Black!
Sasa, hii "wanawake hawapendani" ipo kila Nchi Duniani.....kila mtu anaibuka na sababu yake kwanini hasa hatupendani. Baadhi wanadai ni Wivu wa kike(umbile/kupendeza/mafanikio/kuwa na easylife) na wengine wanasema ni mambo ya Homono tu.
Mie sio kwamba nachukia wanawake bali sipendenzwi na tabia ya baadhi ya wanawake wanaofanya maamuzi ya Kipumbavu, kama vile kutojikinga dhidi ya Mimba, au kujitegeshea kushika Mimba ili tu waolewe au wapate sehemu ya Kipato ya Mwanaume husika. Sipendi mwanamke ajishushe ili kuonewa kirahisi.
Vilevile nachukia wanawake wanaokandamiza wanawake wenzo kutokana na masuala ya kike ili tu waonekane Imara. Unawajua wale wanaoamini kuwa Mimba sio Ugonjwa? au Mwanamke asipozaa basi sio Kamili? ama Mwanamke umeumbwa kuzaa? The shenzi kabisa.
Kutokana na Wimbi kubwa la watu kuachana, kumekuwa na Kesi nyingi kutoka kwa Wanawake wakidai Baba wa watoto wao kuwatunza wao na watoto wao. Hizi Kesi zinaweza kuwa Complicated (inategemea na chanzo cha kuachana, asili ya uhusiano, Umri wa Uhusiano na Mali mlizokusanya mlipokuwa pamoja n.k).
Lakini Majaji wengi wa Kike(Wanawake) wamekuwa wakilaumiwa kuwa na Chuki dhidi ya Wanawake wenzao kwa sababu hawaruhusu Wanaume kutoa pesa za kutosha kwa ajili ya watoto na wao(mamaz). Wanawake wanaamini kuwa kulea watoto ni kazi ngumu (nakubaliana na hili) na hivyo kama Baba hayupo "kimwili" basi Mfuko/Bank acc yake inapaswa kuchangia "ugumu" wa kule watoto wao.
Wanawake wengi wanaegemea zaidi kwenye Chuki "asilia" ya wanawake kwa wanawake. Mie nasema sio chuki bali Wanawake hao(Majaji) wanajaribu kutoa ujumbe(wengi hutoa somo mwisho wa Hukumu) unaofanana na, acha uzembe wa kutaka kutunzwa (via pesa zake) na mwanaume ambae hapati "matunzo" kutoka kwako(ni Ex) na badala yake nenda katafute pesa zako ujitunze mwenyewe.
Sawa, Watoto wana Haki ya kutunzwa/lelewa na wazazi wote wawili wenye Mapenzi sawia(au zaidi kwa one another) lakini likitokea la kutokea au in your case(sorry hihihihi) ulijitegeshea basi usitegemee kuishi kwa kutumia Kipato cha Mwanaume ambae hayupo nawe.
Majaji wengi wanawatoto na hakika walichukua muda kulea watoto wao walipokuwa wadogo kisha wakarudi Kazini/Shuleni. Wengine walisaidiwa na Walezi kwenye Vituo vya kulelea watoto iwe Nursery au Nyumbani kwa mtu au kwa Ndugu na Jamaa. Hakika hii ni personal choice, lakini kama wao waliweza kufanya hivyo kwanini wewe ushindwe?
Weka mfano mzuri kwa kwa Watoto wako kuwa wewe ni Mama Imara na huitaji Mwanaume ili kuishi/kujipenda/kupendeza/kuvutia/kujenga. Muonyeshe Ex wako kuwa Unaweza kuishi Maisha Bora zaidi bila yeye.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments