Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mwanamkeimara

Wanawake hatupendani....usimbee awe Jaji sasa!

Sina hakika kama hii ni Imani tu au ni kweli, Naturally Wanawake hawanipendi mie binafsi(imagine ningekuwa mzuri sasa!) ila Wanaume wanananipenda(napatana zaidi na Wakibaba kuliko Wakimama). Kuna siku Mfanyakazi mwenzangu akanijia kwenye Dawati langu akanambia "dinah unajua nakuchukia".....mie nkacheka halafu nikamwambia "sio peke yako, nimezoea kuchukiwa na wanawake"....wewe ungesema is because i am Black! Sasa, hii "wanawake hawapendani" ipo kila Nchi Duniani.....kila mtu anaibuka na sababu yake kwanini hasa hatupendani. Baadhi wanadai ni Wivu wa kike(umbile/kupendeza/mafanikio/kuwa na easylife) na wengine wanasema ni mambo ya Homono tu. Mie sio kwamba nachukia wanawake bali sipendenzwi na tabia ya baadhi ya wanawake wanaofanya maamuzi ya Kipumbavu, kama vile kutojikinga dhidi ya Mimba, au kujitegeshea kushika Mimba ili tu waolewe au wapate sehemu ya Kipato ya Mwanaume husika. Sipendi mwanamke ajishushe ili kuonewa kirahisi. Vilevile