...Mara nyingi watu husema au kuamini kuwa Mtu anapopata Pesa au Kazi mpya inayolipa Vizuri kuliko kazi yake ya Awali huwa anabadilika(nadhani niliwahi kuzungumzia kwanini watu huwa hivyo mwaka jana/juzi). Habari? natumai Uumzima wa Afya.
Nirahisi kutodhani kuwa Mtu Mzima hawezi kuwa "influenced" na Mtu au Watu wapya wanaomzunguuka....kwasababu amepita Umri wa miaka 30...lakini kihalisia bado wapo Watu Wazima ambao wamekua Miili tu na Namba zimeongezeka lakini Akili zao bado ni za Kitoto. Bado wanapata hitaji la kutaka kufanana, ku-fit in, kuwa kama yule/huyu,kukubalika n.k.
Inasemekana hali hiyo hutokana na Ukosefu fulani wa "attention" kutoka kwa Walezi/Wazazi kipindi ambacho Mhusika alikuwa chini ya Miaka 10. Kumbuka matokeo ya Malezi tuliyopata kutoka kwa Wazazi/Walezi wetu huwa yanaathiri maamuzi (mabaya/mazuri) na Maisha yetu ukubwani. Mtu anahitaji kitu kidogo tu ku-triger alichokosa Utotoni. Achana na hili.
Sasa kwa baadhi mabadiliko huwa Wazi mara tu wanapoanza "Shughuli mpya" hivyo ni rahisi kumuweka Mwenzio sawa na hivyo unakuwa umemsaidia kugundua "mapungufu" yake ambayo yanaathiri Uhusiano/Ndoa yenu.
Wakati mwingine inakuwa ngumu kugundua tofauti (hasa kwa Wanawake) kutokana na Uchovu wa Shughuli zisizoisha za Nyumbani na Malezi ya watoto. Uchovu huo unaweza kukufanya ujishtukie na hata kujibebesha mzigo wa Lawama kuwa wewe ndio sababu ya mabadiliko ya Mwenza wako.
Utakuwa na bahati sana ikiwa Mwaka umepita tangu apate Kazi Mpya/Cheo/Mshahara Mzuri na Mwenza wako hajakutamkia kuwa "umebadilika sana", Jirekebishe, "Humueshimu", "hukuwa hivi siku za nyuma" bla-bla-bla. Sasa leo nitakupa au kukusaidia kuweza kugundua kuwa Mwenza wako aliepata Kazi Mpya au kupanda Cheo na Mwenye Mshahara Mzuri sio yule uliemjua tangu apate kazi Mpya au kupandishwa Cheo.
1)-Ukilalamika kuwa "leo umechoka", yeye atakuambia umefanya nini siku nzima? badala ya kukupa pole na ku-offer msaada au Massage. Kana kwamba shughuli uliyonayo sio muhimu na haichoshi kama yake. Hivyo ni yeye tu ndio anapaswa kuchoka. Na siku akilalama kachoka basi atategemea umfanyie kila kitu kama Binti/Bwana Mfalme.
2)-Anakuwa Mkosoaji kwenye kila jambo unalofanya/taka kufanya au anatoa Jibu ambalo sio "Possitive" kabla hujamaliza kusema/uliza ulichotaka kusema/uliza.
3)-Anapokuwa na siku za Mapumziko anatumia Muda wake huo kuongea na Rafiki zake badala ya kukusaidia vijishughuli viwli vitatu vya Malezi ya Watoto wenu(kama mnao). Kucheza na watoto sio Malezi...tambua hilo.
4)-Kila mnapofanya mazungumzo kuhusu Familia yenu lazima atachomeka Jina la Mtu wake ambe ndiye anam-influence na familia yake. Utasikia "hata fulani hivi, alifanya vile, anafanya hivi" n.k.
5)-Ukihitaji afanye/toe Uamuzi wa kufanya jambo fulani Muhimu kwa Familia yenu basi ataambia Usubiri/umuachie yeye kwanza afanye uchunguzi(anaenda kuwakilisha kwa Mtu wake anaem-influence).
6)-Akipatwa na Tatizo mbali na Nyumbani mtu wa kwanza kujua ni yule anaem-influence na sio Watu wa Msaada au Polisi na wewe Mke/Mume mtu ndio sahau...utasimuliwa tu.
7)-Zile Simu za Mara x2 kuangalia Watoto wameshindaje hazipigwi tena, Muda wote unamalizwa na huyo mtu wake anaem-influence.
Je! Ufanye nini ikiwa umegundua kuwa Mumeo/Mkeo "amebadilika" kutokanana kuwa-influenced na Mtu baada ya kupata Kazi Mpya/Pandishwa Cheo? Usikose Post Ijayo.
Nathanimi na kuheshimu muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments