Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mwenza

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak

Sio lazima wote tuseme "Nakupenda"...

...halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya  kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini? Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa  ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo. Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii  kutoka kwake. Wapo ambao hu

Nini Mbadala wa kuomba radhi kwa Mwenza?

Kawaida sisi Wanawake huwa tunanuna pale tunapokoseawa tukitegemea kuwa Jamaa anakereka kwa kuchuniwa na hivyo ama kukuuliza tatizo ni nini ili umpe Risala au straight up agundue kosa alilokufanyia na akuombe Msamaha. Wengine hawajali hata ukiwanunia, wanachukulia ni "mambo ya Wanawake" na Baada ya Muda utakuwa "fine". Wengine hata ukiwaambia kuwa umehisi kuwa amekukosea/umiza hisia zako na hivyo ni vema akuombe radhi bado ataendelea kujitetea, matokeo yake Ugomvi unaibuka. Sasa unakabiliana vipi na Mwenza kama huyu? Kama nilivyogusia kwenye Post iliyopita hapa  Malezi ya Mwenza wako yanahusika zaidi kwenye suala la kukubali Kosa na kuomba radhi. Baadhi ya Wanawake wapo hivyo pia lakini tofauti ni kuwa baadhi yetu huwa tunapewa Elimu ya Awali ya Maisha ya Ndoa hivyo hata kama Mama na Baba walijisahau au hawakujali kutupa malezi mema bado tutajifunza Ukubwani ili kuwa tayari kuishi na Mtu Baki(Mume). Makosa ninayoyazungumzia hapa ni yale madogo-madogo na

Kukabiliana na Mwenza/Mpenzi "mpya" baada ya Miaka kadhaa...

....kwa maana ya yeye kubadilika/shwa na "Rafiki" zake kama niliyogusia Post iliyopita, ikiwa hukuisoma basi bonyeza hapa . Upo salama lakini?....twenzetu! Kwanza kabisa usimwambie kuwa umebadilika, lakini akikujia na mambo mapya ambayo awali hakuwa akipenda/fuatlia then hoji kulikoni? mf: tangu lini Mpenzi unatazama Eastenders? Hee siku hizi unafuatilia hiki/kile? hii itamfanya atambue kuwa unaona mabadiliko. Pili, Jiweke mbali, yaani mbaaaaaali na hao/huyo "Rafiki" unaedhani ana/amembadilisha Mwenza/Mpenzi wako. Usimuulizie, akianza kukupa stori bila kutaja jina la Mhusika, wewe sema tu "tunamzungumzia John"(taja jina la huyo rafikie mpya)? Halafu onyesha kuwa huna "interest" ya kujua zaidi.(hii itafikisha ujumbe na hivyo kuacha stori za huyo mtu/watu). Tatu, Ataanza kutaka kukutanisha wewe na huyo "Rafiki" kwa kisingizio chochote tu, kuanzia "ametualika kama familia" au "anataka kuja kututembelea ili awaone

Pale Mwenza wako anapobadilishwa tabia na "Rafiki"...

...Mara nyingi watu husema au kuamini kuwa Mtu anapopata Pesa au Kazi mpya inayolipa Vizuri kuliko kazi yake ya Awali huwa anabadilika(nadhani niliwahi kuzungumzia kwanini watu huwa hivyo mwaka jana/juzi). Habari? natumai Uumzima wa Afya. Nirahisi kutodhani kuwa Mtu Mzima hawezi kuwa "influenced" na Mtu au Watu wapya wanaomzunguuka....kwasababu amepita Umri wa miaka 30...lakini kihalisia bado wapo Watu Wazima ambao wamekua Miili tu na Namba zimeongezeka lakini Akili zao bado ni za Kitoto. Bado wanapata hitaji la  kutaka kufanana, ku-fit in, kuwa kama yule/huyu,kukubalika n.k. Inasemekana hali hiyo  hutokana na Ukosefu fulani wa "attention" kutoka kwa Walezi/Wazazi kipindi ambacho Mhusika alikuwa chini ya Miaka 10. Kumbuka matokeo ya Malezi  tuliyopata kutoka kwa Wazazi/Walezi wetu  huwa yanaathiri maamuzi (mabaya/mazuri) na Maisha yetu ukubwani. Mtu anahitaji kitu kidogo tu ku-triger alichokosa Utotoni. Achana na hili. Sasa kwa baadhi mabadiliko huwa Waz

Mtindo 1-10 with a twist....(requested)!!

Mwenye Kwao haachi Jadi si eti? Sasa wewe(na wenzako) "mmepitilizishwa" na Umarekani sijui Usasa bin Usawa mnasahau mpaka Jadi zenu na Maana yake...sio mnasahau bali humzijui na hivyo unakurupuka tu na kusema "Kutoa Mahali ni sawa na Kuuzwa/Nunuliwa"....Hujambo lakini? Sasa ni hivi; kuna mitindo Mingi sana na kumfurahisha Mwenza wako wa Kiume kunako Faragha, kama ujuavyo mwaka 2008 niliandika Topic ya Mtindo wa 1-10 na ikiwa hujui basi endelea kusoma ili uweze kujiongezea au kujifunza "kaujuzi". Mtindo wa  "Moja mpaka Kumi" unafanyika katika Mkao wa Kifo cha Mende Mwanamke juu, Ukishakuwa tayari Bibie weka Mzigo ndani na uingie mpaka Mwisho kisha ujilaze sambamba na Mwili wa Mwenza wako ambae ni Mwanaume(nitatumia Mkibaba kuokoa Muda). Wakati upo kwenye Mkao huo tumia Misuli yako ya Uke kubana na kuachia a.k.a "Piga endiketa", baada ya hapo njoo juu na rudi chini(piga takoz hihihihi) mara Kumi....kwamba kila ukienda chini n

Faida za Kumnunia Mwenza wako....

...Habariyo? Wanawake tunajulikana kuwa tunapenda  sana kununa-nuna si eti? Lakini hata Wanaume pia hununa, ila wao huwa hawaiti "kununa" bali "nataka kuwa peke yangu ili nifikirie" au pengine anaweza kukuambia hajisikiii vizuri au anamawazo. Sote tumetofautiana, jambo dogo kwako linaweza kuwa kubwa sana kwangu, hali kadhalika kauli yako ambayo wewe unadhani ni ya kawaida inaweza kuwa Tusi kuu kwa mwenzio na hata kuhatarisha Ndoa/Uhusiano wenu. Inategemea na Malezi/Makuzi, Mazingira, Uzoefu n.k. Wakati mwingine Kununa is all you need! Biga Mnuno kwa Siku 5(ukizidisha Mkeo/Mumeo ataku-cheat hihihihihi siku ya 6 kidate na ya Saba one night stand....Hisabati Muhimu).....the rule(Bibi yangu alisema), nuna  Maximum Siku Tano tu ukizidisha huna Mume/Mke! Kununa huko hupunguza ukaribu kati yenu kama Mke na Mume, unapokea majibu kwa mkato, ukiingia tu ndani, mmoja anahisi usingizi  ghafla hihihihihi....pia hukupa hisia ya "nampenda" lakini sipendezwi

Chunga Ulimi usimuudhi Mpenzi....

Hello! Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Mambo tunayoambiwa tuyafanye kwenye Ndoa ili tuishi kwa Amani ni mengi mno na yanachukua "utambulisho" wetu......halafu vipi kuhusu Ndoa yenye furaha? Mambo kama "usilopokea....soma nyakati kwanza ili usimuudhi mwenza wako", hii inakufanya uwe mtu mwingine na sio wewe.....katika hali halisi ni task itakayokukosesha furaha kwasababu utakuwa unaishi kama mtu mwingine na sio wewe. Unasoma nyakati only kama issue unayotaka kuiwakilisha kwa mwenzio ni ya kubomoa au kujenga Ndoa yenu. Lakini mambo ya kawaida kama vile kutaniana na kuzungumzia watoto hayahitaji "kusoma nyakati". Kingine ni kusema unavyojisikia baada ya kuvumilia vya kutosha.....ujue wakati wote sisi ni wepesi kuona makosa  madogo madogo ya Wenza wetu kuliko kuona yetu(sio rahisi kuona makosa yako). Na ikitokea Mwenza sio mwepesi kukuambia pale unapokosea basi wewe unadhani kuwa ni kawaida tu na unasonga na maisha. Siku yakimfika shingoni anakuambia ras