Wednesday, 5 October 2016

Nini Mbadala wa kuomba radhi kwa Mwenza?


Kawaida sisi Wanawake huwa tunanuna pale tunapokoseawa tukitegemea kuwa Jamaa anakereka kwa kuchuniwa na hivyo ama kukuuliza tatizo ni nini ili umpe Risala au straight up agundue kosa alilokufanyia na akuombe Msamaha.Wengine hawajali hata ukiwanunia, wanachukulia ni "mambo ya Wanawake" na Baada ya Muda utakuwa "fine". Wengine hata ukiwaambia kuwa umehisi kuwa amekukosea/umiza hisia zako na hivyo ni vema akuombe radhi bado ataendelea kujitetea, matokeo yake Ugomvi unaibuka. Sasa unakabiliana vipi na Mwenza kama huyu?Kama nilivyogusia kwenye Post iliyopita hapa Malezi ya Mwenza wako yanahusika zaidi kwenye suala la kukubali Kosa na kuomba radhi. Baadhi ya Wanawake wapo hivyo pia lakini tofauti ni kuwa baadhi yetu huwa tunapewa Elimu ya Awali ya Maisha ya Ndoa hivyo hata kama Mama na Baba walijisahau au hawakujali kutupa malezi mema bado tutajifunza Ukubwani ili kuwa tayari kuishi na Mtu Baki(Mume).Makosa ninayoyazungumzia hapa ni yale madogo-madogo na yanasameheka. Sizungumzii Usaliti wa Uhusiano(which sio kosa ni Ushetani bin Dhambi)....Usaliti hausameheki unless wewe mwenzangu ni Yesu/Mungu!!Kabla hujaanza kumlaumu hajakuomba msamaha, anza kuchunguza Matendo yake kwako tangu mpishane/gombane. pamoja na kuwa umemnunia/chunia je amefanya nini ndani/nje ya nyumba? Mara nyingi utaona anasafisha vyombo, au anapika....inawezekana akafanya Usafi, kaamka mapema na kuwapa watoto kifungua kinywa? kakununulia kijizawadi na kukiweka mahali bila kukusemasha? Mkilala anakukumbatia(halafu wewe unamsukumia mbali), ana-over-sifia Chakula ulichopika ambacho huwa unapika mara 3 kwa Wiki n.k.Ikiwa hajafanya lolote kama nilivyotaja hapo juu basi ujue kuwa haamini/hajui kuwa alichokisema kwako kimekuumiza hisia na unastahili Radhi yake. Kitu cha kwanza kabisa kufanya ikiwa Mwenza wako sio "kuomba Msamaha" kind of a person, ni wewe kuwa Mfano(kama Mzazi kwa Mtoto). Irudishe Issue mezani na uizungumzie tena.


Omba msamaha kwa kumchunia kwa siku kadhaa, ni kwasababu ya Maumivu aliyokusababishia. Ulimnunia ili kufikisha ujumbe kuwa amekukosea na hivyo akuombe Msamaha(ambao hukuupata), mwambie kuwa kama watu Wazima ni Muhimu sana kuwa Mfano kwa Watoto(kama mnao) kwa kugundua Kosa, kukubali Kosa na kuomba Radhi na kurudisha Uhusiano kwenye hali nzuri ili kuishi kwa Amani na Upendo.


Hakika hatokuambia Nisamehe Mke wangu....akijitahidi sana "atasema nimekuelewa basi yaishe", sio kwamba hataki kukuomba Msamaha isipokuwa hawezi na hajui aanzaje kusema "samahani" ni neno ndogo lakini linauzito mkubwa na ndio maana kwa baadhi ya watu huwa ni gumu kulitoa/sema.


Wanaume wengi (hasa wa Kwetu Barani Afrika)huamini kuwa Kuomba Msamaha ni kama vile kujishusha kwa Mwanamke. anaona bora afanye hivyo kwa vitendo kuliko kutamka neno hilo.


Siku nyingine akikukosea, mueleze hapo kwa hapo na hakikisha ni ana kwa ana. Usifoke na wala usionyeshe Hasira....mwambie ulichokifanya/sema kimeniudhi na kuniumiza hisia zangu, ikiwa kama nimekuumiza wakati nakuelezea naomba unisamehe. Endelea hivyo kila mnapopishana na atajifunza umuhimu wa Kuomba radhi.


Njia nyingne na kumfunza Mwenza wako kuomba Msamaha ni kuwatumia Watoto wakati Baba yao yupo around, wakikoseana waambie waombane Msamaha, wakikukosea waambie wakuombe Msamaha, wakimkosea baba yao watume wakaombe Msamaha/Radhi. Kila mara unawaambia watoto waombe Msamaha/Radhi, waeleze umuhimu wake Maishani, hasa maisha ya ukubwani. Itachukua muda lakini atakugua Umuhimu wa kuomba radhi.


Post ijayo nitagusia Mbadala wa kusema "Nakupenda"....Usikose. nathamini na kueshimu Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

No comments: